BancABC YAJUMUIKA NA WATEJA WAKE KUPATA FUTARI
Mgeni rasmi wa hafla futari iliyoandaliwa na Benki ya BancABC kwa wafanyakazi wa makampuni mbalimbali, Sheikh Ismail Mohamed Salim akizungumza na wageni waalikwa (hawapo pichani) wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hotel Kempisk Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Meneja wa Benki ya BancABC
wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi Bwana Zulfikar Chandoo akizungumza na wageni waalikwa wakati wa hafla hiyo iliyofanyika katika Hoteli ya Kempisk Kilimanjaro mwishoni mwa wiki.
Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam akifuturu wakati wa hafla hiyo
BENKI ya BancABC leo hii imeandaa hafla fupi
kujumuika kwa pamoja na wateja wake waliofunga katika kipindi hiki cha mwezi
mtukufu wa Ramadhani ili kupata futari. Hafla hii fupi imefanyika jijini Dar Es
Salaam katika hoteli ya Hyatt Regency Kilimanjaro na imehudhuriwa pia na Sheikh
Ismail Mohamed Salim ambaye alikuwa mgeni wa rasmi.
Akizungumza
katika hafla hii Meneja wa Benki ya BancABC
wa kitengo cha huduma za kibenki kwa makampuni na taasisi Bwana Zulfikar Chandoo alisema kwamba, “BancABC tunathamini mchango mkubwa tunaopata kutoka kwa wateja wetu
na tumeandaa hafla hii fupi ili kujumuika nanyi jioni hii ya leo ili kupata futari.
Kwa kupitia
mkusanyiko kama huu, tunadumisha mahusiano yetu ya kibiashara, tunajiweka
karibu zaidi na marafiki, jamaa na ndugu zetu bila kujali tofauti zetu za
kiutamaduni, imani au kidini”.
Mgeni rasmi wa
hafla hii Sheikh Ismail Mohamed Salim aliwapongeza sana benki ya BancABCkwa kutambua mchango wa wateja wake wanaofunga na kujitolea kuandaa shughuli
hii. Aliwaasa waislamu kumkumbuka Mungu katika shughuli zao za kila siku kwani
huo ndio mwanzo wa mafanikio katika biashara na shughuli nyinginezo za
binadamu. Aliongeza pia, “ Tukio kama hili la Futari, linatupa nafasi ya
kuungana na kutambua mchango muhimu ambao jumuiya ya kiislamu umetoa kwenye
Historia na Urithi wa nchi yetu nzuri ya Tanzania.
Bwana
Zulfikar alimalizia
kwa kusema, “Tunapenda kuwashukuru wateja wetu wote kwa kuchagua BancABC, tunapenda pia kuwakumbusha
wateja wetu watakaosafiri kwenda Macca kwa ajili ya Hijja mji wa Mecca mwezi October mwaka huu, wafike kwenye ofisi
zetu ili wajipatie kadi za VISA za kusafiria. Kadi hii ni njia salama na
kusafiri na fedha zako popote uendapo. Unaweza kujipatia aidha kadi ya malipo
ya kabla ya BancABC VISA cash card au kadi maalumu za kusafiria za
BancABC VISA Travel Money. Kadi hizi ndio njia salama na rahisi ya kubeba fedha
pale mtu anaposafiri nje ya nchi na dunia nzima kwa ujumla”. Aliongezea kuwa,
BancABC ina huduma kabambe ya Kutoa mikopo wa Wajasiriamali kwa vigezo nafuu
zaidi, ambapo wafanya biashara wadogowadogo wanaweza kujipatia mikopo ya kukuza
biashara zao haraka na kwa urahisi zaidi kwani mfanyabiashara haitaji kuweka
dhamana yoyote ili kupata mkopo huo. Tafadhali fika kwenye moja kati ya matawi
yetu ya BancABC yaliyopo Dar es Salaam na Arusha ili upate maelezo zaidi na uanze
kunufaika na huduma za BancABC.
Baadhi ya Wafanyakazi wa BancABC wakipata futari wakati wa hafla hiyo
Post a Comment