EAST AFRICA MABINGWA SAFARI NYAMA CHOMA MKOA WA KILIMANJARO
Mkuu wa
Wilaya ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi(wa pili kulia) akimkabidhi Meneja wa Bar ya
East Africa,Godfrey Mawala(kulia)Kushoto ni Meneja wa Bia ya Safari Lager,
Oscar Shelukindo.Wapili kulia ni Mpishi Mkuu Wilfred William na Meneja Mauzo wa
Moshi, Edmundi Rutaraka
Mashabiki wa
Bar ya East Africa wakishangilia mara baada ya kutangazwa washindi wakati wa
shindano la Safari Nyama Choma lililofanyika katika Viwanja vya CCM Mkoa
Mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi Wetu, Moshi
EAST AFRICA BAR, wametwaa ubingwa wa mashindano ya
Nyama Choma Mkoa wa Moshi, baada ya kuzigaragaza baa nne zilizotinga fainali ya
mashindano hayo yanayodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia ya
Safari Lager.
Kwa kutwaa ubingwa huo katika fainali zilizofanyika
juzi Jumapili kwenye Viwanja vya CCM Mkoa , baa hiyo ilizawadiwa fedha taslim
Sh milioni moja pamoja na cheti.
Waliokuwa mabingwa watetezi wa mashindano hayo mkoani
hapa, Makanyaga Bar, walishika nafasi ya pili na kuondoka na kitita cha Sh
800,000 na cheti, wakati White Star Pub walishika nafasi ya tatu na kupata
zawadi ya Sh 600,000 na cheti.
Walioibuka na nafasi ya nne ni baa ya Forest Bar
iliyozawadiwa Sh 400,000 na cheti, wakati baa ya Lamina ilishika nafasi ya tano
na kuzawadiwa Sh 200,000 na cheti.
Akizungumza kabla ya kumtangaza mshindi, Jaji Mkuu wa
fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kuwa walitoa mafunzo kwa baa zote hizo
juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.
Alivitaja vigezo walivyotumia kupata mshindi kuwa ni
usafi wa mchomaji, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi,
uhifadhi wake na wa vifaa.
Vingine ni uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini
wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Akizungumza kabla ya kumkaribisha mgeni rasmi, Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, alisema kuwa ni fahari kubwa kwa TBL
na bia ya Safari Lager kwa ujumla kufanikisha shindano hilo mkoani ambao ndio
mkoa wa mwisho.
“Tulianza kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa
zinazofaa kuingia katika shindano la nyama choma kwa mkoa huu wa Moshi tukapata
baa hizi tano zilizoingia fainali ambapo leo tutampata mshindi.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama
hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate
nyama bora,” alisema.
Alisema kuwa bia ya Safari Lager ina miaka takriani 36
na bado imeendelea kuwapo hadi sasa ambapo
ndio inayoongoza kwa mauzo.
Kwa upande wake, mgeni rasmi ambaye ni Mkuu wa Wilaya
ya Moshi, Dr.Ibrahim Msengi, aliisifu
TBL kupitia Safari Lager kwa kuandaa mashindano hayo, akisema kuwa serikali
inatambua mchango wa kampuni hiyo katika kujenga uchumi wa Taifa kupitia tukio
hilo na mengineyo kama mashindano ya Pool Safari Lager, Safari Wezesha na hata
udhamini wao katika michezo mbalimbali kama soka na mingineyo.
“Mashindano haya ni mazuri kwani yanawajengea wateja wa
nyama mazingira mazuri na salama katika kutoa huduma hii ya nyama choma,”
alisema.
Alizitaka baa ambazo hazikufika fainali, kutokata tamaa
na badala yake kujipanga kwa ajili ya mashindano ya mwakani, kwa kurekebisha
yale waliyokosea mwaka huu.
Post a Comment