ZAIDI YA MILLION 31.9 ZAGHARAMIA VIFAA LIGI YA MOHAMMED DEWJI, SINGIDA
Mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida
mjini, Hamisi Nguli (kushoto) akikabidhi vifaa vya michezo kwa kiongozi
wa tawi la Mitunduruni.
Foleni ya viongozi wa matawi katika
jimbo la Singida mjini wakikabidhiwa vifaa vya michezo kwa ajili ya timu
zao kushiriki kombe la MO inayotarajiwa kuanza Januari 20 mwaka huu. (Picha zote na Nathaniel Limu).
Mbunge wa jimbo la Singida
mjini,Mohammed Gullam Dewji,ametoa msaada wa vifaa mbalimbali vya
michezo vyenye thamani ya zaidi ya shilingi 31.9 vitakavyotumika kwenye
ligi ya kombe lake, inayotarajiwa kuanza kutimua vumbi januari 20 mwaka
huu.
Vifaa hivyo ni pamoja na jezi pea
854,mipira 122, soksi pea 854 na cloves za magolikipa 61.Vifaa hivyo ni
kwa ajili ya timu zitakazoshiriki ligi ngazi ya kitongoji katika jimbo
la Singida mjini.Baada ya ligi hiyo,itafuatwa na ligi ngazi ya kata
ambayo atakuwa na vifaa vyake pia.
Akizungumza kwenye hafla ya kukabidhi
vifaa hivyo,mwenyekiti wa CCM jimbo la Singida mjini, Hamisi Nguli
amepongeza mbunge Dewji kwa kuendelea kutoa misaada mikubwa mbalimbali
katika jimbo lake kwa lengo la kuendeleza wapiga kura wake na wananchi
kwa ujumla.
“Dewji toka awe mbunge wa jimbo la
Singida mjini,siku zote yupo karibu zaidi na vijana. Amewasaidia mambo
mengi makubwa ikiwemo kuwaendeleza kimichezo na pia ametoa pikipiki kwa
ajili ya vijana wa bodaboda watakaojiunga katika vikundi”,alisema.
Awali msaidizi wa mbunge Dewji, Duda
Mughenyi,amesema msaada huyo wa vifaa,ni mwendelezo wa Dewji kuhakikisha
vijana wanatumia michezo kujiendeleza kimaisha.
Post a Comment