RAIS WA ZANZIBAR DKT. SHEIN AFUNGUA JENGO LA CHUO CHA UTAWALA WA UMMA,TUNGUU ZANZIBAR
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akifungua pazia kama ishara ya ufunguzi wa jengo la Chuo cha Utawala wa Umma, lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja wakati wa hafla ya ufunguzi huo iliyofanyika jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar,(kulia) Waziri wa Utumishi wa Umma na Utawala Bora Haji
Omar Kheir.
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,(wa pili kulia) akifuatana na Waziri wa Utawala wa Umma na Utawala Bora Haji Omar Kheir,(kushoto) pamoja na Viongozi wengine baada ua kulifungua jengo la Chuo cha Utawala wa Umma,lililopo Tunguu Mkoa wa Kusini Unguja jana,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar
Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein, akisalimiana na Mkuu wa Wilaya ya Kati Vuai Mwinyi,alipowasili katika shere za Ufunguzi wa Jengo la Chuo cha Utawala wa Umma,liliopo Tunguu,Wilaya ya Kati Unguja,katika shamra shamra za kilele cha miaka 49 ya Mapinduzi Matukufu ya Zanzibar.
Baadhi ya wanafunzi wa Chuo cha Utawala wa Umma,walioshiriki katika sherehe za ufunguzi wa jengo la Chuo hicho huko Tunguu,Wilaya ya Kati unguja jana,ambapo Rais wa Zanzibar na Mwenyekiti wa Baraza la Mapinduzi Dk. Ali Mohamed Shein,alikuwa Mgeni rasmi.Picha na Ramadhan Othman,Ikulu.
Post a Comment