NDEGE MEDICS YAKABIDHI AMBULANCES ZA KISASA KWA HOSPITALI YA AGA KHAN KWA AJILI YA MRADI WA KUBORESHA AFYA YA MAMA MJAMZITO NA MTOTO TANZANIA
Mwenyekiti
wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi
Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege
wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa
Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama
Mjamzito na Mtoto Tanzania
Head of
Primary Medical Centre Bwa. Siwawi Konteh (wa pili kulia) ambaye pia ni
mratibu wa mradi wa Tuunganishe Mikono Pamoja ili kuokoa Afya ya Mama
na Mtoto akizungumzia Malengo Makuu ya mradi huo kuwa ni kuongeza
kiwango na matumizi ya Huduma ya Afya ya Mama Mjamzito na Watoto na
kushirikiana na kujifunza kuhusu Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto. Kutoka
kushoto ni Acting Medical Director wa Aga Khan Hospital Dr. Ambrose
Chanji, Mwenyekiti wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib,
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Dr. Sebastian Ndege na
Kulia ni Mkuu wa Kitengo cha Rasilimali Watu cha Hospitali hiyo Bw. Anis
Nazrani.
Mkurugenzi Mkuu na Mwenyekiti wa
Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege (wa pili kushoto)
akizungumza wakati wa kukabidhi magari ya kubeba wagonjwa kwa hospitali
ya Aga Khan ambapo amesema vifo kadhaa vinavyotokea katika hospitali
nyingi kwa sasa vinawahusisha akinamama na watoto wasio na hatia ambao
hukosa huduma za awali za haraka zikiwemo usafiri na hivyo katika kujali
hilo wametoa magari hayo.
Aidha amesema Ndege Medics
inashukuru kuwa sehemu ya mradi endelevu wa kujaribu kuokoa maisha ya
akina mama na watoto ambao lengo lake ni kuchangia katika kuboresha afya
ya uzazi wa mama na watoto wachanga katika mikoa ya Dodoma, Iringa,
Mwanza, Mbeya na Morogoro.
Mwenyekiti
wa Bodi ya Hospitali ya Aga Khan Bw. Amin Habib (kushoto) na Mkurugenzi
Mkuu na Mwenyekiti wa Ndege Medics Services Limited Dr. Sebastian Ndege
wakikata utepe kuashiria kukabidhiwa magari ya kubeba wagonjwa kwa
Hospitali ya Aga Khan ikiwa ni katika mradi wa kuboresha Afya ya Mama
Mjamzito na Mtoto Tanzania
Wakipongezana baada ya makabidhiano hayo.
Mmoja wa wafanyakazi wa Ndege Medics akionyesha baadhi ya vifaa vilivyomo ndani ya magari hayo ya kisasa.
Pichani
Juu na Chini ni muonekano wa magari hayo ya kubebea wagonjwa kwa ndani
yaliyotelwa kwa hospitali ya Aga Khan na NDEGE Medics kwa ajili ya mradi
wa kuboresha Afya ya Mama Mjamzito na Mtoto Tanzania.
Post a Comment