Tamasha Kuhamasisha Ngumi Mtwara
Bakari dunda akivishwa mkanda na mbunge wa mtwara baada ya kuchukuwa ubingwa huo katika ukumbi wa makonde
Tamasha la kuhamasisha masumbwi mkoani mtwara lilimalizika kwa
mafanikio mazuri kwa watu kuitikia na kukubali mapambano mengine mengi
ya ngumi kufanyika mkoani humo.
katika tamasha hilo lililosindikizwa na pambano la ubingwa wa taifa
la uzito wa unyoya kati ya Bakari mohamed'dunda wa blackmamba ya mtwara
alimshinda abdala seleman wa dar es salaam,
Nae mkongwe Rashid 'snake man" matumla alimshinda kiaina yake
bondia Patrick amote wa kenya katika pambano ambalo liliwasimua sana
mashabiki na kuwafanya kushindwa kukaa vitini muda wote wa pambano na
hasa pale mkenya alipokwenda chini kwa konde zito lililotupwa na matumla
baada ya kukwepa ngumi na kutupa hilo konde kwa kushtukiza,mwanzo
alianza taratibu na kuonekana kama mchovu kutokana na kitambi
alichonacho na kujikwaakwaa ulingoni lakini kadiri muda ulivyosogea
ndivyo alivyobadirika na kuonekana mzuri zaidi.
pambano jingine lililowaacha hoi wapenzi wa mtwara na kukaa kimyaaa
na kuduwaa kwa mshangao ni la haruna mnyalukolo wa dar na ashraf wa
blacmamba kwani ngumi zilipoanza tu walianza kwa nguvu sana na kutupiana
makonde mfululizo yaliyomuingia kila mmoja na kupelekana chini kwa zamu
na wote walivimba nyuso na kutokwa na damu baada ya kupasukapasuka
mpaka mwishowe ashraf spidi na uvumilivu ulipomshinda na kukubali
kuliachia pambano kwa kukataa kurudi ulingoni raundi ya nne pambano
lilikuwa la raundi sita.
Post a Comment