KOCHA WA NGUMI C. MZAZI KUWAPOZA MACHUNGU MABONDIA WALIODHURUMIWA NA PROMOTA KAIKE
Kocha
wa ngumi za kulipwa Christopher Mzazi, kutoka Gym ya "No Ttalking" ya
Mabibo ya jijini Dar es Salaam, ameamua kuwapoza machungu mabondia
chipukizi, Mwaite Juma na Baina Mazola, waliowahi kupiganishwa na
Promota, Kaike na kisha kuwadhurumu malipo yao ya pambano hilo.
Mabondia
hao wanatarajia kupanda Ulingoni Novemba 18/2012 huko maeneo ya Mabibo
katika ukumbi wa D.I.D, ambapo pambano hilo litakuwa ni la upinzani
kubwa kutoka na mabondia hao kutambia na kufikia kutaka kuzichapa kavu
kavu mtaani.
Akilizungumzia
pambano hilo kocha mzazi alisema kuwa mabondia hao wote ni wazuri ambao
wanaofundishwa na kocha mzuri mwenye uwezo mkubwa pia ni mabondia
wazuri
na ni tegemeo zuri la baadae.
''Sielewi ni kwanini Kaike aliamua kuwafanyia
uhuni na kuwadhurumu, hivyo mimi nikiwa kama mzazi kama jina langu
nimeona ni vyema nikawapoza machungu kwa kuwapa pambano na mabondia wangu
na kuwalipa zaidi ya pesa walizodhurumiwa kwa kuwa ninaelewa machungu na ugumu wa mchezo wenyewe ulivyo''. alisema mzazi.
Hivyo
basi Mwaite Juma, kutoka BigRight boxing gym atacheza na Baina Mazola wa
No talking gym katika pambano la raundi nane.
Na Pambano hilo kali litasindikizwa na Karim
Ramadhan (mdogo wa Nasibu Ramadhan-bondia bora wa mwaka) atakaecheza
na Martin Richard.
Siku
hiyo pia kutakuwa na mapambano mengi ya kiushindani ya kuwekana sawa
nani zaidi ya mwingine kati ya mabondia wa mabibo na mwananyamala.
Post a Comment