Vita vya Majimaji na harakati za uhuru wa Tanganyika
Na Abdallah Mbonde.
DESEMBA 9,mwaka huu nchi yetu Tanganyika(Tanzania bara)itaadhimisha miaka 49 ya uhuru tuliupata toka kwa mkoloni wa Kiingereza mwaka 1961.
Uhuru huo ulipatikana baada ya harakati nyingi na za muda mrefu zilizoshirikisha watu na vikundi mbalimbali vya kisaiasa na kijamii katika kupanga mikakati ya kuung'oa utawala wa kijerumani na baadaye Uingereza.
Miongoni mwa harakati hizo ni zile za vita vya Majimaji zilizoanzishwa na wanachi wa kabila la Wamatumbi,kijijini Nandete,Tarafa ya Kipatimu,wilaya ya Kilwa mkoani Lindi.
Kwa kuzinagatia hilo nimeona ni vyema na haki tukakumbushana na kuona jinsi gani wananchi hao wa kabila hilo na jamii ya makabila mengine kusini mwa nchi yetu walivyoshiriki mapambano dhidi ya utawala wa kikatili,ukandamizaji,utesaji na kila aina ya uovu wa Serikali ya kikoloni ya Kijerumani.
Baada ya mgawanyo wa bara letu la Afrika au bara la giza kama walivyozoea kuliita wakoloni wa nchi za Ulaya nchi yetu Tanganyika iliangukia mikononi mwa Ujerumani.
Utawala huo wa Kijerumani ulianzisha kilimo cha Pamba kama zao la biashara ili kupata malighafi kwa ajili ya kuendeshea viwanda vyao huko kwao na kujenga uwezo wa kuiimarisha utawala wao nchini.
Nini Kilisababisha hasa vita hivyo?
Mzee Issa Ndenge Mbonde(87)mmiliki wa Sehemu iliyojengwa mnara wa kumukumbu ya vita hivyo na chanzo cha vita hivyo hukuo Nandete anasimulia kuwa.
Wamatumbi walishikwa kwa nguvu kutoka katika maeneo yao ya koo mbalimbali nyumba hadi nyumba walimokuwa wakikaa bila ya ridhaa yao.
Kukamatwa huko kulihusisha vitendo vya udhalilishaji mbele ya familai zao na wananchi hao kulazimika kuziacha familia na mashamba yao na kupelekwa kulima kwenye mashamba ya Pamba yaliyokuwa yanamilikiwa na Wajerumani.
Mshamba hayo yalikua katika maeneo ya vijiji vya Nandete,Mundi,Mwengei,Mtumbei Kitambi na wengine kupelekwa kwenye mashamba yaliyokuwepo huko Somanga katika eneo la pwani ya bahari ya Hindi.
Huko mashambani walishurutishwa kazi za shuruba za kuyahudumia mashamba hayo,kufyeka misitu,kupanda,kupalilia na kuvuna.
Kazi hiyo ya kilimo cha Pamba haikuwa ya malipo wala maafikiano yoyote.Wakati huo huo walitakiwa kulipa kodi ya kichwa (Hut taxi)iliyokuwa imeanzishwa na Wajerumani na kumtaka kila mtu mzima kulipa.
Kwa mila na desturi ya Wamatumbi siyo waoga wa kilimo,lakini kule kushurutishwa na kusimamiwa huku wakichapwa viboko ilihali wakijua wazi kwamba mazao hayo ya Pamba hayana maslahi kwao na hata kwa maendeleo ya Tarafa yao kuliwafanya wazinduke na kupanga mikakati ya kuung'oa utawala mzima wa Wajerumani.
Wamatumbi hao waliwasoma vya kutosha Wajerumani kuwa wameingia nchini Tanganyika kinyemela kwa lengo la kuendeleza utawala wao uwe imara na wa kudumu ili wapate mazao ya kilimo kwa uwingi na kusafirishwa kwao.
Wazalendo walikuwa vitendea kazi wa wakoloni hao na si kwa maendeleo yao.
Kama vile haitoshi wakati wa mavuno ya Pamba hiyo waligeuzwa kuwa Wapagazi(Manamba)kubeba marobota ya pamba kutoka maeneo ya kilimo mashambani kupeleka Kikanda(Njia nne)kilipokuwa kiwanda cha kuchambulia pamba.
Walitembea kwa miguu mchana kutwa,usiku kucha kupitia vijiji vya Kibata makao makuu ya Serikali hiyo(Boma)katika eneo hilo,Pungutini,Kinjumbi,Somanaga hadi Kikanda.
Pamba iliyokwisha chambuliwa hapo Kikanda ilibebwa tena kwenye marobota na kupelekwa kwenye bandari ya Matapatapa iliyopo katika pwani ya bahari ya Hindi ili isafirishwe kwenda ulaya.
Mkusanyiko huo mkubwa wa koo mbalimbali za Wamatumbi uliyokuwepo pale Nandete na maeneo mengine ya vijiji vya Mwengei,Mtumbei Kitambi na Mundi yalikokuwepo mashamba makubwa ya Pamba ya Wajerumaniilisababisha wananchi hao kupata maarifa mapya.
Na kwa vile walishikwa kwa nguvu na kufanyizwa kazi kwa shuruba na tena bila ya malipo,walijiona kunyanyaswa na kudhalilishwa mno.
Siyo hivyo tu bali pia walijiona wamevunjiwa heshima,haki na utu kutokana na kuwepo kwa ukandamizwaji mkubwa waliokuwa wanaupata kutoka kwa watawala wa Wajerumani.
Hali hiyo ilizua manung'uniko na minong'ono na kujitokeza chuki kubwa na uhasama ukajengeka dhidi ya Wajerumani na vibaraka wao.
Hali hiyo ilisababisha wananchi hao kumwona kila mzungu ni adui yao hata kama mzungu huo si Mjerumani.Balaa kubwa!
Hivyo pole pole kwa usiri mkubwa wakaanza mazingira ya kujipanga vyema na kuanza michakato ya kupanga mbinu ya kuutokomeza utawala huo wa Wajerumani.
Wamatumbi walifahamu fika umahiri na uwezo mkubwa waliokuwa nao Wajerumani kivita na pia kufahamu wanazo silaha kali za moto.
Lakini kila walivyofikiria mateso makubwa waliyokuwa wakiyapata toka kwa Wajerumani hao walijipa moyo na kushikwa na nguvu ya ajabu na hivyo kuamua njia pekee ya kuung'oa utawala huo wa Wajerumani na walowezi(Settlers)wao ni kupambana kivita.
Uhamasishaji,ushirikishwaji na harakati za hapa na pale zikaaza,mazoezi ya kivita(Likinda)yakaanza kwa kasi na usiri mkubwa sana pale Nandete.
Walipojiaona wanaharakati wengi kujitokeza na wengi kuitikia wito wa kuwa tayari kwa mapigano ya kuung'oa utawala wa Kijerumani hivyo mwaka 1904/05,Nandete pakateuliwa kuwa mchakato wa kupanga jinsi ya kuung'oa utawala wa Ujerumani.
Mchakato huo ni pamoja na utoaji wa mafunzo ya kivita(Likinda),utaratibu wa upatikanaji na utengenezaji wa silaha(mikuki,mundu/mbopo.mashoka,mishale,visu,na ngumbewe,rungu/ndonga nk).
Utaratibu wa upatikanaji wa vyakula na tiba kwa ajili ya wapiganaji watakaoumia au kuumwa wakati wa mapigano uliandaliwa vizuri sambamba na tiba za jadi zinazohusu kinga na miiko ili wasidhurike na silaha yoyote ile kutoka kwa maadui zao Wajerumani kwa imani iliyotolewa kutoka kwa jopo la ufundi.
Mojawapo katika kuonyesha msimamo,mshikamano na umoja wa hali ya juu hapo Nandete katika kipindi hicho cha harakati waanzilishi na wapiganaji hao wa vita ya Majimaji wakapathibitisha ndipo yawepo makao makuu ya jeshi la Wazalendo na kituo kikuu cha uratibu wa vita hivyo.
Walipojua wako vyema kivita na kupata ujasiri wa kupambana na Wajerumani,wakaanza chokochoko ndogondogo za kupinga hiki na kile na migomo ili mradi wajerumani waadhibu na hivyo iwe sababu ya kuanza vita.
Walipoona kwa makosa hayo waliyokuwa wanafanya hawadhibiwi waliona kama wanacheleweshwa muda wa kuanza vita.
Wakanza kutumia mbinu zingine ndipo Julai 15,1905 pale Nandete wakaamua kufanya tendo la kipekee ambalo walikuwa na uhakika Wajerumani watakasirika sana na watachukua hataua za haraka iwe ni stahili ya kuanza kung'oa Pamba kwenye mashamba ya Serikali ya Wajerumani.
Hatua hiyo ilichukuliwa ili kuwakasirisha Wajerumani na vita ianze mara moja kwani zao la Pamba lilikuwa na muhimu mkubwa katika kuimarisha utawala wao na walifanikiwa.
Baada ya wanaharakati kuona Wajerumani tayari wamekasirika na wamechachamaa na sasa wanataka kuangamiza,la mgambo likapigwa na wakereketwa wote wa Umatumbi ya kwamba vita ile iliyokuwa inasubiriwa sasa imeanza wavae nguo za kivita(Manjenga)wabebe kila aina ya silaha waliyokuwa nayo na kila mmoja awe katika kikosi chake vitani.Witikio ulikuwa mzuri mno.
Kutokana na uwepo wao uliyokuwepo na mkusanyiko mkubwa pale Nandete na kutokana na kila mmoja kupata uhamasishaji na kupewa mafunzo ya kivita,baada tu ya tendo la kung'oa pamba kufanyika kijijini Nandete wanaharakati wakawa tayari kila mmoja kujiunga kwenye kikosi chake na kuamriawa kwa ujasiri wasonge mbele kuelekea Kibata na kuteka Ngome kuu ya Wajerumani na kuutokomeza utawala wao.
Ndipo vita vya Majimaji vikanza rasmi Julai 15, 1905.
Hakika,wanaharakati na wapiganaji hawa walikuwa ni watetezi wa haki na kujikomboa dhidi ya utwala mbaya wa kikoloni wa Kijerumani iliyokuwa imeanzishwa mwaka 1884 nchini Tanganyika.
Kutokana na kuwa na ari na nguvu mpya mapigano ya vita hivyo yalizidi kuwa makali,vita vilisikika na kuungwa mkono na makabila mbalimbali.
Hatimaye Vita hivyo vilisambaa sehemu kubwa kusini mwa Tanganyika ambako leo hii kuna mikoa ya Lindi na Mtwara na kusambaa kwa makabila ya Wangindo,huko Njinjo na Liwale,Wamwera.
Baadaye hadi kwa Wayao,Wamakua(Masasi)Wangoni,Wandendeule na Wamatengo(Ruvuma)Wabena na Wapangwa (Njombe)Wapogoro(Mahenge)Wambunga,Wandamba(Kilombero),Wandengereko wa Mbwara(Rufiji)wazaramo na Wavidunda toka Kisarawe.
Baada ya mapigano ya miaka miwili kupita kukatangazwa rasmi Agosti 8,1907 na Serekali ya Wajerumani kumalizika kwa vita hivyo vya ukombozi wa mwafrika na Ujerumani kujitangazia ushindi.
Wamatumbi hao wanaheshimiwa sana kwa sababu hawakuwahi kuanzisha mapigano ya vita miongoni mwa koo zao mbalimbali au kwa makabila yaliyokua yanapakana nayo kwa kutaka himaya yao.
Badala yake walikusanyika na kuelekeza nguvu zao za kishujaa kwenye kupinga utawala ulikuwa mbaya wa Taifa la kigeni la Kijerumani lililokuwa linatawala Tanaganyika kimabavu.
Turejee kwenye historia ya chanzo cha vita vya Majimaji na jinsi mapigano yalivyoenea utaona jinsi gani na kwa saikolojia ipi ilitumika na Wamatumbi ambao waliweza kufanya mahusiano na makabila ya kusini mwa Tanganyika na hivyo kuungwa mkono na kuelezea dhamiya yao ya kuung'oa utwala wa Kijerumani nchini Tanganyika.
Matokea baada ya vita Waume,Wake na watoto walipotezana,walikosa malazi na makazi ya kudumu ya kuishi.
Hali hiyo ilitokea kwa sababu miji mbalimbali ilisambaratishwa na kikosi cha Fyeka fyeka kilichoongozwa na Meja Johannes na wenzake Kepteni Mortz Merker,Lt Spiegel na staff Surgeon England wakiwa na maamluki(askari wa kukodi wapatao 200 kutoka Sudan(Wanubi)na kuchoma moto mashamba,mazao na miti ya matunda.
Magonjwa ya kila aina.hapakuwa na tiba hata ile ya kijadi,watoto na akina mama walifariki kwa njaa.
Watu wengi walipotea hasa katika harakati za kulikomboa boma la Kibata
Unaweza kustajabu kwa nini Kenjeketile hajazungumzwa katika makala haye kama kiongozi wa vita hivyo.
Mila na desturi za kabila hilo la Wamatumbi halina uchifu kila mtu na familia yake ni chifu ndio maana na ndivyo ilivyokuwa Kenjekitile hakuwa chifu wa kabila hilo ila ni mganga wa jadi maarufu wa tiba ya kupiga bao,Maoka/mizimu kinga za magonjwa na mazingaombwe.
Mganga huyo alisaidia sana jopo la ufundi liliongozwa na bibi Ntabila Naupunda,Siikwaku Mbonde,Ngulumbalyo Mandai,Mpilaa Ndutui Kipengele,Mataka Nkwera Mwiru na wengineo.
Inasimuliwa Kinjeketile alishikwa na utawala wa Kijerumani kabla ya vita kuanza na wakampeleka kifungoni Muhoro,Rufiji na kumnyonga Agosti 5 1905 hivyo hakujihusisha na vita hivyo moja kwa moja ,wajerumani walipata taarifa zake mapema juu ya tiba na shughuli zake za uganga.
Katika kuenzi na kukumbuka harakati hizo za kabila la Wamatumbi katika ukombozi wa Tanganyika umejengwa mnara wa mashujaa katika Kijiji cha Nandete mahali ilipoanzia vita hivyo wilayani Kilwa ,mkoani Lindi na kuzinduliwa na mheshimiwa Rais Jakaya Mrisho Kikwete Agosti mwaka huu.
Hali kadhalika kwenye kikao cha mkutano wa TANU(Tanganyika African National Union) kilichofanyika mkoani Mwanza mwaka 1967,Baba wa Taifa Mwl Julius K Nyerere aliwaomba wajumbe wa mkutano kusimama na kuwakumbuka wapiganaji wa vita vya Majimaji kwani walikuwa "Wadai wa kwanza wa Uhuru nchini Tanaganyika"
"Bendera ya Mwingereza inateremshwa na ya Mmatumbi inapandishwa"hayo ni baadhi ya maneno ya mtangazaji wa Tanganyika Broadcasting Service(TBS) Hamza Kasongo siku ya Uhuru wa Tanganyika Desemba 9,1961.
Maoni 0716 801987 au domolangu@hotmail.com

Post a Comment