ad

ad

*ABUU SEMHANDO AFARIKI KWA AJALI DAR

Baadhi wa wasanii wa bendi ya Twanga, na wasamaliawema, wakipakia mwili wa marehemu katika gari.

PATA PICHA ZA TUKIO HILO LA KUSIKITISHA NA HUZUNI.

ALIYEKUWA mpiga Dram mahiri wa bendi ya African Stars (Twanga Pepeta) Abuu Semhando, maarufu kama Baba Diana, amefariki dunia usiku wa kuamkia jana kwa kugongwa na gari maeneo ya Mbezi Beach Tangibovu wakati akitoka kwenye onyesho la bendi yao lililofanyika kwenye Ukumbi wa Afrikana Pub.

Semhando amegongwa na gari ndogo aina ya Benzi lenye namba za usajiri T 855 BLQ, ambalo pia liliingia mtaroni na dereva kutokomea pasipojulikana baada ya ajali hiyo.

Mashuhuda wa ajali hiyo alieleza kuwa ajali hiyo ilitokea mida ya saa nane kasoro usiku eneo hilo, baada ya gari hilo kumgonga kwa nyuma marehemu na kusha kumburuza umbali wa kama mita 30.

“Sie tumeona tu gari hili likimburuza baada ya kumgonga na aliporushwa barabarni magari mengine ndiyo hasa yaliyommalizia kwa kumpanda mara kadhaa kwani alikuwa hajiwezi hata kuinuka tena na pia ni muda mrefu kidogo toka itokee ajali hii bila kupata msaada magari yote yalikuwa yakipita tu hadi walipoanza kufika jamaa zake” alieleza mmoja wa walinzi wa usiku anayelinda maeneo hayo muda huo ukiwa ni saa kumi kasoro.

Akielezea matukio ya marehemu dakika chache kabla ya ajali hiyo, Mnenguaji wa bendi hiyo, Super Nyamwela, alisema kuwa muda mchache kabla ya tukio hilo wakati wakiwa katika onyesho lao, marehemu alikuwa akipanda jukwaani na kumtunza Nyamwela kwa kutoa noti za Sh. 10,000 na kumdai chenji jambo ambalo alilifanya mara kadhaa ukumbini hapo ambavyo si kawaida yake kufanya utani wa namna hiyo.

“Alikuwa akinitunza fedha mara kadhaa jukwaani huku akisimama na kunidai chenji wakati mie nikiendelea kucheza namie nilikuwa nikimhesabia chenji yake na kumrudishia huku akicheka utani ambao hakuwahi kuufanya na pindi alipomaliza kufanya hivyo aliondoka ukumbini kabla yetu akielekea nyumbani kwake Mwananyamala na dakika chache tu tunapata taarifa ya kifo chake na kukimbia eneo hili la tukio na kukuta ajali hii” alisema Nyamwela

Baada ya ajali hiyo mwili wa marehemu ulichukuliwa na gari la kubebea wagonjwa la Kampuni ya Night Suport, kuekea Kituo cha Polisi Oysterbay kabla ya kupekwa kuhifadhiwa Hospitali. kwa habari zilizopatika zimeeleza kuwa Semhando anatarajia kusafirishwa kesho alfajiri kuelekea Muheza Tanga kwa mazishi..
Hili ndilo Gari lililomgonga na Marehemu Aduu Semhando hadi kufa.
Hapa ni wakati wakisubiri gari kuja kupakia mwili wa marehemu

No comments