VODACOM YAZINDUA MASHINDANO YA MBIO ZA BAISKELI JIJINI DAR.
MASHINDANO ya baiskeli yanatarajiwa kufanyika mjini Mwanza, Novemba 12 hadi 13 na kudhaminiwa na Kampuni ya Simu za Mikononi ya Vodacom, huku yakigharimu shilingi Milioni 50.
Akizungumza na waandishi wa habari jana jijini Dar es Salaam, Mkuu wa Udhamini wa Vodacom Tanzania, George Rwehumbiza, alisema kwamba mashindano hayo yameboreshwa kwa kiasi kikubwa.
Alisema kwamba waendesha baiskeli wajitokeze kwa wingi katika patashika hizo huku akisema yatakuwa na tija na faida kwa mchezo huo.
“Mashindano hayo yatafanyika kwa siku mbili Novemba 12 na 13, huku yakiwa ni mbio za kilomita 196 kwa wanaume, kilomita 80 kwa wanawake, huku walemavu wanaume wakishiriki mbio za kilomita 15 na wasichana kilomita 10.
“Shindano hili la Vodacom Mwanza Cycle Challenge ni mahususi kwa kukuza mchezo huu hapa nchini kwa lengo la kupata wawakilishi bora katika mashindano mbalimbali ya kimataifa,” alisema.
Mashindano hayo yanaandaliwa kwa mwaka wa tano na Vodacom Tanzania, huku yakidhaminiwa na Alphatel, TBL, Knigth Support na SBC, kupitia kinywaji chake cha Pepsi.
Post a Comment