ad

ad

MAKONGO KULA EID NA WATOTO YATIMA

MAKONGO KULA EID NA YATIMA
SHULE ya Sekondari ya Makongo jijini Dar es Salaam imejumuika na kituo cha kulelea Watoto yatima cha New Life Orphans kilichopo Kigogo katika kusherehekea Sikukuu ya Eid jana.

Akizungumza na Watoto Rais wa Interact Club,Mbisso Joseph ambaye ni Mwanafunzi wa shule hiyo alisema wao kama wawakilishi wa wanafunzi wa Shule yao wakishirikiana na Uongozi wa Shule hiyo wanatambua uwepo wa Watoto Yatima na ndio maana wameguswa kujumuika nao kwa kubadilishana mawazo na kuwapa zawadi mbalimbali za Sikukuu ya Eid.

Katibu Mkuu wa Klabu hiyo,Salome Solomoni alianisha zawadi hizo kuwa ni Mchele kilo 50,Unga kilo 50,Sukari,Mafuta ya kupikia,Sabuni,Machungwa,Biscuti,Vifaa vya Shule na Nguo.

Kwa niaba ya Mkuu wa Shule,Kapteni Mstaafu,Hamis Mfaume aliwashukuru wanafunzi kwanza kwa kufikiria kitu kama hicho kwani ni mfano mzuri kwa jamii na kwa wanafunzi wenzao kwa kutambua uhitaji wa Watoto wenzao.

Nae Mwalimu,John Ngowi kwa niaba ya waalimu wa Makongo aliushukuru uongozi kwa mlezi mazuri mara baada ya kupata taarifa ya kituo hicho haswa kwa kuwaendeleza watoto ki Elimu Dunia nia Ahela.

Alisema Ngowi kwa furaha mara baada ya kupata taarifa kuwa kuna watoto wawili kutoka katika kituo hicho wanasoma makongo,sikutegemea,huu ni mwanzo walioonyesha wanafunzi wetu hivyo tunaahidi kutoa ushirikiano zaidi hasa kwenye swala la Elimu alimaliza Ngowi.

Kwa niaba ya watoto yatima,Issa Athumani alishukuru kwa kitendo walichoonyesha na kuwataka isiwe mara ya mwisho,hivyo wamefurahi sana na wanawakaribisha tena muda wowote.

Kituo cha New Life Orphans kina jumla ya Watoto 104,kati yao wa kike ni 35 na wakiume ni 69.Walioko Sekondari ni 16 na kati yao 12 walifaulu wenyewe alisema Patroni wa kituo,Mwinyi Khatibu.

Mwisho wanafunzi walishukuru kwa mapokezi na kuahidi kuushawishi Uongozi wa Shule ya Makongo kusaidia kuwasomesha watoto hao wanaofikia Sekondari kama sio bure basi hata kwa kuchangia gharama kidogo kupitia wafadhiri wao alimaliza Rais wao Mbisso.

Wanafunzi na Waakimu wa Shule ya Sekondari ya Makongo wakiwasili kwenye kituo cha kulelea Watoto Yatima cha New Life Orphans kilichopo Kigogo jijini Dar es Salaam.

Wakibadilishana mawazo na watoto hao.

Huyo Mtoto aliyebebwa ni moja ya Watoto ya tima wa kituo hicho.





Rais wa Interact Klabu ya Makongo,Mbisso Joseph akimkabidhi mmoja wa watoto yatima kwa niaba ya wote moja ya zawadi walizowapelekea
Akimkabidhi


Mbisso akizungumza kilicho wasukuma kutembelea kituo hicho.

Picha ya Pamoja.

Patroni wa kituo,Hamis Khatibu mwenyekanzu akishukuru.


Dua
Kaptani Mtaafu,Hamis Mfaume akiongoza Dua.
Dua

1 comment

Anonymous said...

My name is Mbisso Josephat,i wish to come again in the future. I was the President of the club in 2010/12. God bless you all