ZIARA YA WAANDISHI WA HABARI NAMBARA KIKWE WILAYANI MERU KUTEMBELEA MIRADI ILIYOFADHILIWA NA HEIFER.
Wanakijiji wa Mambara wakifundishwa mbinu mbalimbali za Ufugaji na Kilimo hai na Joseph Masoud ambaye ni matunda ya Heifer
Wanakijiji wakimsikiliza kwa makini.
Anna Masoud akizungumza na waandishi wa habari walipokuwa wamemtembelea kujua amefaidika vipi na Heifer,Familia hii inamafanikio makubwa kutokana na Heifer,kwa mara ya kwanza ilipata Mbuzi wa maziwa kutoka Heifer ikapokea na elimu ya ufugaji, Ng'ombe na Mbuzi na samaki na pia kilimo hai ambapo mpaka sasa kutokana na Mbuzi wana mbuzi 8,Ng'ombe,Kuku,wanalima Mahindi na Kilimo hai na pia wanabwawa la Samaki.Wana familia ya Watoto 4,na wote wako shule na wanamlea Mtoto Yatima ambaye walikwenda kumuomba kwenye kituo cha kulelea Watoto Yatima ikiwa ni shukrani kwa mwenyezi Mungu kwani mpaka mafanikio waliyonayo walipata bure na wao hawana budi kumrudishia MWENYEZI MUNGU.Kwa sasa wanajenga mtugi wa kuzalisha umeme wa Gas ambao bila Heifer wasingeweza.
Hawa ni kuku wa kienyeji ambao pia ni matunda ya Heifer.
Huyo ndiye Mtoto yatima wanamlea wakiamini ni shukrani kwa Mwenyezi MUNGU.Wakiwaonyesha waandishi wa habari sehemu ya Kilimo hai.
Huyu ni Nguruwe ambaye ni matunda ya Heifer
Hili ni Bwawa la Samaki ambalo pia ni matunda ya Heifer
Post a Comment