ad

ad

Dullah Mbabe alonga, si ngumi tu, hata soccer naweza.

 Mchezaji wa timu ya Dame Boxing, Boxer, Abdallah Pazi “Dullah Mbabe”(kulia) akikabiliwa na walinzi wawili wa timu ya Wakuvesha zote za Mwananyamala wakati wa Bonanza lililoandaliwa na Vijana CCM Tawai la Mwanjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam.Timu ya Wakuvesha ilishinda 2-1.




 Mchezaji wa timu ya Dame Boxing, Boxer, Abdallah Pazi “Dullah Mbabe akijaribu kufunga dhidi ya timu ya Wakuvesha zote za Mwananyamala wakati wa Bonanza lililoandaliwa na Vijana CCM Tawai la Mwanjuma Mwananyamala jijini Dar es Salaam. Timu ya Wakuvesha ilishinda 2-1.



Na Mwandishi Wetu.
Boxer, Abdallah Pazi( Dullah Mbabe) amebambwa kitaa akicheza Soccer mitaa ya Mwananyamala katika Uwanja wa CCM Mwinjuma lililoandaliwa na Vijana wa CCM wa Tawi hilo mwishoni mwa wiki.
Katika Bonanza hilo, Dullah Mbabe alikuwa akichezea timu ya Dame Boxing akihudumu kama namaba tisa,ambapo katika mechi yao ya awali dhidi ya Wakuvesha walifungwa 2-1.
Mechi ya pili timu ya Dame Boxing ilicheza na timu ya Gereji ambapo timu ya Dame Boxing ilishinda 3-0, magoli mawili yalifungwa na Dullah Mbabe.
Akizungumza na mwandishi wetu, Dullah Mbabe alitamba kuwa mimi si Boxing tu bali hujumuika pia na ndugu na marafiki kufanya mazoezi ya mpira wa miguu, “Lakini leo tuna Bonanza hapa ambapo timu itakayoshinda inazawadiwa Mbuzi mmoja” alisema Dullah Mbabe.
Bonanza hilo lilijumuisha timu mbalimbali za mitaa ya Mwananyamala lengo ikiwa kuleta mshikamano kama Vijana wa eneo moja lakini pia kuhamasishana kufanya mazoezi kwani michezo ni afya, michezo huleta kufahamiana.
Dullah Mbabe kwa sasa anajiandaa na mpambano  wa IBF unaotarajia kufanyika Nchini China hivyo anatarajia kusafiri April 24, mwaka huu kueleke China.

No comments