ad

ad

CASTLE LAGER KUWAPELEKA WATANZANIA ‘WORLD CUP’

 Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli (katikati) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside).yaliyofanyika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam.Kulia ni Meneja Masoko ,Habari ,Udhamini na Promosheni za wateja, George Kavishe na Balozi wa Kampeni hiyo, Ivo Mapunda.

Kampuni ya Bia Tanzania (TBL) kupitia kinywaji chake cha Bia ya Castle Lager, imezindua rasmi mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside).
Mashindano haya yenye hadhi ya kimataifa yanashirikisha timu za wachezaji watano (5) kila upande, na kocha mmoja. Mechi zake zitakuwa zikichezwa kwa dakika saba (7) ili kata mshindi.
Bingwa wa michuano hiyo ataiwakilisha Tanzania huko Zambia katika michuano ya kimataifa dhidi ya nchi nyingine 5 kutoka Afrika ambazo ni: Afrika Kusini, Zambia, Zimbabwe, Swaziland, Lesotho. Baada ya hapo mshindi atapata fursa ya kwenda Urusi kushuhudia michuano ya Kombe la Dunia baadaye mwaka huu, akiambatana na mashabiki wawili ambao watapatikana katika mchakato malumu pamoja na mchezaji mmoja mkongwe kutoka nchi ambayo ni bingwa. Kama Tanzania itafanikiwa kushinda, timu pamoja na mashabiki hao wawili wataongozana na mkongwe katika soka Ivo Mapunda aliyekua kipa wa Taifa Stars na Simba Sports Club.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar es Salaam, Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli, alisema kuwa, kuna michakato maalumu ya kupata timu shiriki kupitia katika baa mbalimbali jijini Dar es Salaam.
“Utaratibu wa kupata timu utawahusisha moja kwa moja mashabiki wa baa husika kupendekeza timu zao, kabla ya hatua nyingine za kuzipigia kura timu zinazotakiwa kushiriki. Mteja wetu atapata maelekezo maalumu kutoka kwa watu wetu ambao watakuwa wakipita katika baa hizo kwa nyakati tofauti. Sifa kubwa ya mteja wetu kushiriki katika mchakato huo ni pamoja na kununua bia ya Castle Lager,” alisema Kikuli.
Akitolea maelezo za ziada jinsi mchakato huo wa Castle Lager Africa 5s utakavyokua, Meneja Masoko, Udhamini na Promosheni za Wateja George Kavishe amesema kua, michuano hiyo inashirikisha baa 160, zitakazogawanywa katika makundi 10, huku kila kundi likiwa na baa 16. Kila kundi litatakiwa kuwa na kiwanja chake katika michuano ya awali ya timu 16 na kupata timu 8. Wilaya zote za Mkoa wa Dar es Salaam zitashiriki katika michuano hii. Hapa tukimaanisha Kinondoni, Ilala, Temeke, Ubungo na Kigamboni. Bonanza za kuanza kuchagua timu wakilishi za wilaya zitaanza tarehe 17 Machi hadi 21 Aprili kisha Bonanza kuu itakayoleta timu 10 za fainali itakua tarehe 28 Aprili 2018.
“Katika hatua ya pili ya bonanza tutapata timu moja kutoka katika yale makundi 10 ya awali na kufikisha idadi ya timu 10 zitakazocheza katika bonanza kubwa pale Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam, kupata timu tano (5) zitakazocheza kwa mtindo wa ligi na hatimaye kupata bingwa.” Alisema Meneja Kavishe.

Michuano hii inafanyika kwa miezi miwili, ambapo washiriki wanatakiwa kuwa na umri wa miaka kati ya 24 na 34. Lengo la mashindano haya ni kuwaleta pamoja marafiki na mashabiki wa soka. Wachezaji walioko katika ligi mbalimbali nchini hawatoruhusiwa kushiriki katika michuano hii, hata kama wana kigezo cha umri uliotajwa hapo juu.                                                           
Meneja Masoko ,Habari ,Udhamini na Promosheni za wateja, George Kavishe(kulia) akizungumza na waandishi wa habari wakati wa uzinduzi wa mashindano maalumu ya soka yanayofahamika kama ‘Castle Lager Africa 5s’ (5 – Aside).yaliyofanyika Viwanja vya Leaders jijini Dar es Salaam. Katikati ni Meneja wa Bia ya Castle Lager, Pamela Kikuli.
 Balozi wa Castle Lager 5s, Ivo Mapunda akizungumza
 . Meneja Masoko ,Habari ,Udhamini na Promosheni za wateja, George Kavishe(kushoto) akipiga Penati  kuashilia uzinduzi wa Promosheni ya Castle Lager 5s uliofanyika Leaders.Kulia ni Balozi wa Kampeni hiyo, Ivo Mapunda.
 Meneja Masoko ,Habari ,Udhamini na Promosheni za wateja, George Kavishe(kushoto) akisalimiana na wachezaji wakati wa uzinduzi wa uzinduzi wa Promosheni ya Castle Lager 5s uliofanyika Leaders.Kulia ni Balozi wa Kampeni hiyo, Ivo Mapunda.

No comments