Huawei, Skytel wazindua duka kubwa Arusha
Afisa
Biashara wa jiji la Arusha, Steven Sultan(wa pili kulia) na Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin(wapili
kushoto) wakikata utepe kuashilia uzinduzi wa duka la Huawei Skytel uliofanyika
leo jijini Arusha.Kuhoto ni Meneja Huawei Kanda Kanda ya Kaskazini, Betrice
Vitalis.
Afisa
Biashara wa jiji la Arusha, Steven Sultan(wa pili kulia) na Meneja wa Huawei jijini Arusha,Qin Yilin(wapili
kushoto) wakipongezana kwa kushikana mikono mara baada ya kukata utepe
kuashilia uzinduzi wa duka la Huawei Skytel uliofanyika leo jijini
Arusha.Kuhoto ni Meneja Huawei Kanda Kanda ya Kaskazini, Betrice Vitalis.
Meneja Huawei Kanda Kanda ya
Kaskazini, Betrice Vitalis(kushoto) akitoa maelekezo ya bidhaa za Huawei kwa fisa Biashara wa jiji la Arusha,
Steven Sultan mara baada ya uzinduzi wa
Duka ka Huawei Skytel kuzinduliwa rasmi jijini Arusha leo.Kulia ni Meneja wa
Huawei jijini Arusha,Qin Yilin na Mkurugenzi wa Duka hilo, Bobkevin Shoo.
KAMPUNI ya Teknolojia ya Mawasiliano ya Huawei
Tanzania kwa kushirikiana na Mfanyabiashara maarufu wa simu jijini Arusha, Skytel
wamefungua duka kubwa liitwalo “ Huawei Skytel Brand Shop” katika Jiji la
Arusha. Hatua hiyo ni mwendelezo wa Huawei katika kutekeleza moja ya mikakati
yake ya kujitanua kibiashara nchini.
Huawei imeona kuwepo wa Duka hili kubwa la Skytel, katika Jiji la Arusha
kunatokana na kukua mahitaji ya bidhaa za Huawei nchini na hivyo kutoa fursa ya
watumiaji kupata huduma kwa karibu zaidi.
“Tunafahamu watanzania walio wengi wanachohitaji, ndiyo maana leo hii
tuko Jijini Arusha. Tunaamini kuwa hii ni fursa pekee kwa wakazi wa Arusha na
miji ya jirani kupata bidhaa zetu zenye ubora na viwango vya hali ya juu.
Tunaamini kuwa Skytel wana jina kubwa katika Jiji la Arusha na hivyo
itatusaidia sisi kutimiza lengo letu, alisema Meneja wa Huawei jijini
Arusha,Qin Yilin.
Mwaka huu kampuni hii ya simu ilijipanga kusambaza huduma yao nchi
nzima, sambamba na kufungua maduka kwaajili ya kusogeza huduma zetu kwa wateja.
Hali hii imetuongezea wepesi wa utoaji wa huduma zao kwa kufanikiwa kwa kiasi
kikubwa kutambua mahitaji muhimu kwa wateja wetu,
Tanzania imefaidika na uhusiano mzuri uliopo kati yake na Huawei kwa
kuwa na miradi mbalimbali yenye lengo la kuboresha teknolojia ya mawasiliano.
Huawei inampango wa kukuza teknolojia ya mawasiliano nchini Tanzania na sasa imeanza
kushirikiaba kwa karibu na wazawa kama Skytel. Milango iko wazi kwa yeyote
anayetaka kutuunga mkono kiabiashara.
Wakati Huawei inazindua duka hilo katika Ukanda wa Kanda Kaskazini, Meneja
wa Huawei Arusha alitangaza uwepo wa simu mpya ya kisasa, Huawei Y3II na
nyinginezo, katika soko la simu nchini.
Alisema kuwa simu hiyo ina ubora na kuwataka watanzania kutumia,
akifafanua zaidi kuwa ni simu yenye ubora, lakini gharama yake sio kubwa,
ikilinganishwa na simu za makampuni mengine.Pia bidhaa nyingine zitaambatana na
simu hiyo kama matoleo mangine tofauti Huawei P9, Y3c, Y5II ,Y6II, Y3lite na
nyingine nyingi.
Hizi ndizo faida za kuwa na duka kubwa katika Jiji la Arusha. Kuanzia
sasa wanunuzi wa bidhaa zetu wana fursa ya kupata bidhaa zetu zote kwa wakati. Tunaanza
na simu hii ya Huawei Y3II ambayo kwa hakika kila atakayeamua kuitumia
ataipenda kwa ubora wake.
Kwa mujibu wa Meneja huyo, Kampuni ya Huawei inaendelea na mchakato
wake wa kusogeza huduma zake kwa wateja wake, kwa lengo la kutimiza malengo
yake ili kupambana na soko la mawasiliano.
Post a Comment