Asifa
mnadhimu wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Mwandamizi wa Polisi
Fortunatus Musilimu akiwakabidhi Oil za
Total 4T madereva boda boda mala baada ya uzinduzi rasmi wa vilainishi
hivyo.Hafla ya Uzinduzi ilifanyika Viwanja vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar
es Salaam.
Asifa
mnadhimu wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Mwandamizi wa Polisi
Fortunatus Musilimu akiwakabidhi Kofia
maalumu za kuendeshea Pikipiki(Helmeti) madereva boda boda mala baada ya
uzinduzi rasmi wa vilainishi vya Tatal 4T.Hafla ya Uzinduzi ilifanyika Viwanja
vya Mwembe Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
 |
Asifa
mnadhimu wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Mwandamizi wa Polisi
Fortunatus Musilimu akiwa kwenye picha
ya pamoja na madereva Bodaboda mara baada ya uzinduzi wa vilainishi maalumu vya
Pikipiki na bajaji vya Tatal 4T.Hafla ya Uzinduzi ilifanyika Viwanja vya Mwembe
Yanga Temeke jijini Dar es Salaam.
Total Tanzania yazindua bidhaa mpya “Special 4T”, kilainishi mahsusi
kwa ajili ya pikipiki na bajaji.
Katika harakati za kuwafikia wateja wake wote, kwa kuwapa huduma na
bidhaa zenye uhakika, Total Tanzania imezindua kilainishi kipya nchini, kijulikanacho kama Special
4T, ambacho ni mahususi kwa ajili ya
pikipiki na bajaji zenye “4 stroke engine”.
Kilainishi hiki cha SPECIAL 4T hulinda
injini ya bodaboda na bajaji, na kuzuia msuguano
kati ya vipuri na kifanya injini kuwa nyepesi na mwendo wa kasi pia kuiwezesha
kufanya kazi kwa muda mrefu Zaidi bila kuharibika. Hivyo kuwasaidia wamiliki wa
bajaji na bodaboda kupunguza gharama ya kufanya matengenezo mara kwa mara. Tunawashauri wamiliki wa
Bodaboda na Bajaji watumie kilainishi hiki cha SPECIAL 4T ya TOTAL ambacho
kitawawezesha kufanya safari za umbali wa kilomita kati ya 2200 mpaka 2500 bila
kubadilisha ( Oil drainage period)
Uzinduzi huu wa bidhaa mpya ni matokeo ya utafiti uliofanywa na wataalamu
wa kampuni ya TOTAL kwa baadhi ya waendesha bodaboda na bajaji na kugundua kuwa
madereva na wamiliki wengi hutumia vyombo vyao kwa biashara hivyo hutembea
umbali mrefu na kufanya injini kuchakaa na kuwa dhaifu mara kwa mara kwa
kutumia vilainishi visivyo na viwango bora. Hivyo hutumia gharama kubwa zaidi
kufanya matengenezo
Akizungumza kwenye uzinduzi huo, Meneja Mauzo wa Vilainishi na bidhaa maalumu za Total,
Bwana Anam Mwemutsi alisema; “lengo letu ni kumsaidia mmiliki wa bodaboda na bajaji kuweza kufanya biashara
zake kwa gharama nafuu bila hofu ya kuharibika kwa injini. Tumeleta kilainishi
ambacho hakitamlazimu kufanya matengenezo kwa chombo chake mara kwa mara, kwa sababu
itamruhusu kutembea kilometa nyingi bila kubadilisha. Na kutokana na ubora wa bidhaa zetu, tunamhakikishia mteja uimara
na ulinzi kamili wa injini yake wakati wowote na kwenye barabara yoyote ile
Tanzania nzima“
Bidhaa hii ya SPECIAL 4T itapatikana katika vituo vyote vya mafuta vyaTotal
na kwa mawakala wetu waliothibitishwa nchi nzima.
“Ningependa kuwashukuru Total kwa kuja na bidhaa hii. Kwa ubora wake utasaidia
kupunguza gharama za uendeshaji wa biashara kwa waendesha pikipiki na bajaji. Ila
pia nawasihi waendesha bodaboda kufuata alama za barabarani, kuvaa kofia ngumu
na kuvaa reflectors ili kuweza kujikinga na ajali wawapo barabarani”
alizungumza mgeni rasmi Ofisa mnadhim wa Jeshi la Polisi Nchini, Kamishna Msaidizi wa Polisi, Fortunas Musilimu.
Kuhusu
Vilainishi vya Total
Total ni wasambazaji wa vilainishi mbalimbali vya magari, vyombo vya
majini, mitambo na mashine za viwandani na za kilimo. Vilainishi hivi
vimetengenezwa kwa ufanisi mkubwa ili kuwezesha injini ya chombo chako kuhimili
hali ya hewa ya aina yoyote ile iwe joto au kipindi cha mvua kali. Vilainishi
vya Total huimarisha, hulainisha, hupunguza msuguano na kuipa nguvu injini ya
chombo husika kufanya kazi kwa muda mrefu zaidi bila kuchoka wala kuchakaa.
|
Post a Comment