TOT sasa waja kivingine.
Muimbaji wa
Bendi ta TOT, Abdul Misambano akiimba sambamba na waimbaji wengine wakati wa
onyesho lao la kila ijumaa katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Rapa wa
Bendi ya TOT, Issa Sadi akiimba sambamba na wanenguaji wa bendi hiyo wakati wa
onyesho lao la kila ijumaa katika Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es
Salaam mwishoni mwa wiki.
Na Mwandishi
Wetu.
BENDI ya TOT
yenye makazi yake Mkuu CCM Mwinjuma, Mwananyamala jijini Dar es Salaam, imekuja
kivingine mara baada ya pilika pilika za Chama cha Mapinduzi kumalizika kwa
kutoa burudani kwa wapenzi na mashabiki wa Dansi na Taarabu katika Ukumbi wao
wa CCM Mwinjuma kila Ijumaa ikiwa ni sehemu ya kuihakikishia jamii kuwa hawako
kichama tu bali kuna maisha baada ya Chama.
Akizungumza
na waandishi wa habari msemaji wa Bend Frank Kabatano alisema kwa sasa TOT
Bandi na Taarabu tuko katika maisha mengine kabisa baada ya siasa
kumalizika.Tumeanza na ukumbi wa nyumbani kwa sasa kila ijumaa tutatoa burudani
mbili kwa pamoja yaani Taarabu na Mziki wa Dansi yote hiyo ni katika
kuwahakikishia wapenzi kuwa hatuko kwa ajili ya Chama tu bali hata jamii nzima
bila kujali kabila jinsia wa itikadi.
Alisema
Kabatano, TOT Band kwa sasa inatamba na nyimbo zake mpya kama; Wivu utunzi wake
Abdul Misambano, Pilipili utunzi wake Msemaji wa Bendi Frank Kabatano, Acha
kulia utunzi wake J4, Afidhi utunzi wake
Athanas Monthanabe na zingine nyingi.
Wakati
upande wa Taarabu ukiongozwa na Malkia wa Mipasho Tanzanaia, Khadija Koppa
akitamba na nyimbo zake mpya kibao bila kuacha nyimbo yake ya “Naheshimu kazi
yangu ndio inayoniweka mjini” utunzi wake mwenyewe na zingine nyingi.
Alisema
Kabatano, ni wakati sasa wa wapenzi wa Taarabu na mziki wa Dansi kuja kuona na
kusikiliza burudani kutoka TOT ili upate radha nyingine ya pekee ambayo
hujawahi kupata.
Wiki hii
Bandi ya TOT wakatakuwa kiwanja cha nyumbani tena CCM Mwinjuma, Mwananyamala na
wakati huo huo jumapili watakuwa na Bonanza hapo hapo CCM Mwinjuma.
Waimbaji wa
Taarabu wa Bendi ya TOT wakicheza wakati wa onyesho lao la kila ijumaa katika
Ukumbi wa CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki.
Wanenguaji
wa Bendi ya TOT wakicheza wakati wa onyesho lao la kila ijumaa katika Ukumbi wa
CCM Mwinjuma Mwananyamala Dar es Salaam mwishoni mwa wiki. |
Post a Comment