UTATA WAZIDI KUTANDA UMRI NA UHALALI WA MISS TANZANIA 2014
Baada
ya kuonekana kuwa mrembo wa taji la Miss Tanzania 2014, Sitti Mtemvu,
amedanga kuhusu umri wake halali aliotakiwa kutaja ili Kamati ya
mashindano ya Miss Tanzania iweze kumruhusu kushiriki mashindano hayo au
la, wadau wa tasnia ya urembo wanaomfahamu kwa karibu mrembo huyo
wamekuwa wakizidi kutoa baadhi ya vidhibitisho vya mrembo huyo
vinavyoonyesha umri halisi ambao ni miaka 25 badala ya ile 18
aliyoitaja.
Aidha
wadau hao wamezidi kwenda mbali zaidi kwa kuweka picha ya mrembo huyo
inayoonyesha akiwa na mtoto wake jambo ambalo linazidi kuichanganya
kamati ya mashindano hayo kwa kuona kuwa tayari huu ni mwaka wa tabu na
kashfa kubwa kwao ambayo haijawahi kutokea tangu kuanzishwa kwa
mashindano hayo.
Japo
inawezekana ilishawahi kutokea kwa warembo kudanganya kuhusu umri na
kuwa na watoto, lakini haikuweza kuwa na kishindo na kuvuta hisia za
wengi kama ilivyo kwa mrembo huyu wa 2014.
Kwa
mawazo ya wadau wengi wa tasnia ya urembo, wamekuwa wakishauri kuwa ni
bora kamati husika ikae chini na kuchukua maamuzi magumu ya kumvua taji
hilo mrembo huyo na kumkabidhi mshindi wa pili, ili kuendelea kulinda
heshima ya mashindano hayo ambayo kwa uhakika yanaelekea kupoteza mvuto
na mwelekeo na hasa kutokana na kashfa kama hizi.
Pichani
ni moja ya picha zilizopostiwa na watu wa karibu wa mrembo huyo kuwa
eti huyo aliye naye pichani ni mtoto wake, habari ambayo haina uhakika
ila ni kwa mujibu wa mitandao.
Post a Comment