SAFARI LAGER YAZINDUA RASMI PROGAMU YAKE YA “SAFARI LAGER WEZESHWA” KWA MSIMU IV, 2014.
Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kushoto) akiwaonyesha kipeperushi cha
shilingi 2200,000 000/= zitakazogawiwa kwa wajasiliamali wakati wa uzinduzi wa
prpgramu ya Safari Wezeshwa msimu wan ne uliofanyika jijini Dar es Salaam. Kulia
ni Jaji wa programu hiyo, Joseph Mmigunda.
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja
wa bia ya Safari Lager Bw. Oscar Shelukindo
alifafanuwa ya kwamba “ programu hii ni hazina tosha kwa wajasiriamali wadogowadogo
nchini kwani itarahisisha kazi kwa
kuwepo na vitendea kazi bila ya kutumia nguvu nyingi”.
Programu hii ni msimu wa nne tangu kuanzishwa kwake na imeleta mafanikio makubwa kwa wajasiriamali
waliopata uthubutu wa kujaribu kujiunga na hatimae kuongeza uchumi wa nchi.
Bw. Oscar alifafanuwa kuwa, Programu hii itafanyika takribani mikoa yote
Nchini ambapo fomu zitaanza kutolewa kuanzia leo kupitia mtandao wa www.wezeshwa.co.tz na baadae kusambazwa
katika mabohari na viwanda vya TBL nchi nzima.Hii itawapa fursa wajasiriamali wa
aina zote bila kujali fani,kabila wala jinsia kujaza fomu kwa usahihi na
kamilifu kisha kuzirudisha mahala husika na baadae waliokidhi nafasi
zinazohitajika kuchaguliwa kisha kupewa mafunzo mafupi pamoja na kukabidhiwa ruzuku zao.
Nae Jaji kutoka TABDS, Bwana Joseph Migunda alisema kuwa “Zoezi hili linahusisha majaji wenye utaalamu
na wenye umakini kwa namna moja au nyingine.Hivyo aliomba
wajasiriamali wote wenye nia ya kufika mbali kibiashara na wenye malengo ya kuisaidia jamii inayowazunguka wasisite
kuchangamkia fursa hii”.
Post a Comment