NDOVU SPECIAL MALT YAZINDUA “NDOVU GOLDEN EXPERIENCE”
Meneja wa
Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya “Ndovu Golden Experiece”
yenye lengo la kumlinda mnyama Tembo iliyofanyia Dar es Salaam jana.Kulia ni
Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah
Meneja wa
Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya “Ndovu Golden
Experiece” yenye lengo la kumlinda mnyama Tembo iliyofanyia Dar es Salaam jana.Kushoto
kwa Pamela ni Meneja Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah na
warembo wa Ndovu Special Malt.
Meneja
Masoko wa Kampuni ya Bia Tanzania, Fimbo Butallah akionyesha namna ya kushiriki
kampeni ya Ndovu Golden Experience kwa waandishi wa habari(hawapo pichani) wakati
wa uzinduzi wa kampeni maalumu ya “Ndovu Golden Experiece” yenye lengo la
kumlinda mnyama Tembo iliyofanyia Dar es Salaam jana.Kulia kwa Fimbo ni Meneja
wa Bia ya Ndovu Special Malt, Pamela Kikuli na warembo wa Ndovu Special Malt.
NDOVU Special Malt leo hii imezindua kampeni yake kabambe ijulikanayo kama“Ndovu
Golden Experience” ambapo itawazawadia watumiaji wa bia ya Ndovu zawadi kubwa
ya kufanya matembezi ya utalii wa ndani nchini Tanzania.
Akizungumza na wandishi wa habari, Meneja wa bia ya Ndovu Special Malt Bi. Pamela
Kikuli alisema “ Utalii ni sekta muhimu sana katika nchi yetu hususani katika
kukuza uchumi wa nchi ingawa kuna watalii
wengi sana kutoka nje ya nchi wenye muamko mkubwa kuliko watanzania. Kwa sasa kampeni ya “Ndovu Golden Experience”
imetoa fursa kwa Watanzania kufanya
utalii wa ndani ili kujionea maajabu mazuri
katika nchi yetu kwa kutembelea hifadhi za Seleous.
Bi. Pamela alienedela kufafanua na
kusema, Kampeni hii ya bia ya Ndovu Special Malt inayojulikana kama “Ndovu
Golden Experience” inategemea kuanza
katikati ya mwezi octoba mwaka huu ambapo kila wiki atapatikana mshindi
mmoja atakayejipatia nafasi mbili za kutembelea mbuga za Selous, gharama zote
zimelipiwa na bia ya Ndovu. Ili kushiriki katika shindano hili mtumiaji wa
kinywaji cha Ndovu Special Malt anapaswa kutuma namba maalum ziilizowekwa chini
ya kizibo cha bia ya Ndovu Special Mallt na kuzituma kwa SMS kwenda namba 15499 au kwa njia ya tovuti kupitia www.ndovuspecialmalt.com/goldenexperience. Maelezo
haya ya jinsi ya kushiriki yanapatikana pia kupitia nembo (lebo) ya nyumba ya
bia ya Ndovu.
Meneja wa masoko wa TBL Bw. Fimbo Butallah aliongeza kwa kusema kuwa “ kampeni ya ‘Ndovu Golden
Experinece’ ni muendelezo wa kampeni tuliyoanza nayo mwaka jana inayoujulikana
kama Ndovu Defenders au Walinzi wa Tembo. Kampeni hii ilifanyika kupitia
mitandao yetu ya kijamii ili kuwahamasisha na kusambaza elimu kwa Watanzania
kuhusu ujangili dhidi ya Tembo, na mshindi wake pia alizawadiwa safari ya watu
wawili ya kwenda kutembelea hifadhii zetu maarufu za wanyama za Selous. Na sasa
hii kampeni ya ‘The Ndovu Golden Experience’ kwa mara nyingine inawapa nafasi watanzania
ya kufanya utalii wa ndani na hapo tunaamini kuwa watapata motisha ya kulinda
mali asili zetu, wakiwemo Tembo.
|
Post a Comment