Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tekinologia ya Huawei Tanzania, Vincent Wen(kushoto) akizungumza
na washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano ulioanza
jana katika Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa HUAWEI.
Mkurugenzi
wa Kampuni ya Tekinologia ya Huawei Tanzania, Vincent Wen akizungumza na
washiriki wa Mkutano wa Kimataifa wa Tekinolojia ya Mawasiliano(hawapo pichani)
wakati wa ufunguzi ulioanza jana katika
Hoteli ya Bahari Beach jijini Dar es Salaam kwa udhamini wa HUAWEI.
Washiriki wa
mkutano huo.
Washiriki wa
mkutano huo.
 |
Na mwandishi wetu
MAMLAKA ya Udhibiti wa Mawasiliano Tanzania (TCRA) inatarajia kuupitia upya utaratibu wa malipo ya vifurushi vya muda wa maongezi ili kumwezisha mtumiaji kuvitumia bila ukomo.
Hayo yalisemwa jana jijini Dar es Salaam na Mkurugenzi Mtendaji wa TCRA, Prof. John Mkoma wakati wa Mkutano wa Kimataifa wa pili wa Mawasiliano Kusini, Kati na Mashariki mwa Afrika.
Mkutano huo uliratibiwa na Shirika la Mawasiliano nchini(TTCL), Huawei na Mkongo wa Taifa (NICTBB).
Prof. Mkoma alisema, taasisi yake imepokea malalamiko juu ya muda wa ukomo wa vifurushi mbalimbali vya muda wa mawasiliano na hivyo tayari wameshaanza kulifanyia kazi.
“Tunataka mawasiliano rahisi kwa wananchi, swala hili tumelipokea na tunalifanyia kazi,” alisema na kubainisha kuwa “ni muhimu wananchi wakajua umuhimu wa vifurushi mbalimbali kabla ya kujiunga,” alisema Prof. Mkoma.
Naye Mkurugezi Mtendaji wa Shirika la Mawasiliano nchini (TTCL), Dr. Kamugisha Kazaura alisema mkutano huo wa siku mbili unashirikisha washiriki zaidi ya 230 kutoka Afrika na nje ya Bara la Afrika.
Dr. Kazaura alisema kupitia katika mkutano huo wadau wa sekta ya mawasiliano kutoka nchi za Afrika na nje ya Afrika wanapata fursa ya kukutana pamoja na kubadilishana mawazo jinsi ya kuboresha sekta hiyo.
Alisema kupitia katika mkonga wa taifa tayari wameziunganisha nchi zote za Afrika Mashariki na Kati na zilizo jirani isipokuwa Malawi.
Katibu Mkuu wa Wizara ya Mawasiliano, Sayansi na Teknolojia, Prof.Patrick Makungu ambaye alimwakilisha waziri wa wizara hiyo, Prof. Makame Mbalawa alisema mkutano huo kufanyika Tanzania ni jambo la kujivunia kwa Watanzania kutokana na kwamba inaonyesha jinsi gani nchi ilivyopiga hatua katika sekta ya mawasiliano.
Prof. Makungu alisema mkutano huo unawaunganisha wahitaji na watoa huduma ya mawasiliano kwa nchi za Afrika na nje ya Bara la Afrika.
Afisa wa Huawei alisema, kampuni yake itaendelea kufanya kazi na Mfuko wa Mawasiliano kwa Wote (UCSAF) ili kuwezesha ufanisi wa mawasiliano sehemu za vijijini.
Aliongeza kuwa, wadau wa mawasiliano na makampuni mbalimbali kwa kushirikiana na serikali, pamoja inawezekana kuboresha mawasiliano nchini.
|
Post a Comment