Katibu
Mkuu wa Chama cha Pool Taifa, Amos Kafwinga akimkabidhi Nahodha wa timu ya Top
Land kitita cha fedha taslimu Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014
kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam
 |
Wachezaji
wa timu ya Top Land wakishangilia kwa kucheza
na kitita cha Shilingi 800,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa mashindano ya Safari Pool 2014
kwa Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni jijini Dar es Salaam
Na Mwandishi
Wetu.
MABINGWA
watetezi klabu ya mchezo wa Pool ya Top Land ya Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni
jijini Dar es Salaam imemefanikiwa kutetea
Ubingwa wake katika fainali za
mashindano ya mchezo huo yajulikanayo kama “Safari National Pool Competition
2014” kwa kuwafunga timu ya klabu ya Meeda 13-5, yaliyomalizika mwishoni mwa
wiki Mkoani humo na kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 800,000/= pamoja na tiketi
ya kuwakilisha Mkoa wa kimichezo wa Kinondoni kwenye fainali za kitaifa zinazotarajiwa
kufanyika Mkoani Kilimanjaro.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa na Meeda Pool Klabu na kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi
400,000/= na nafasi ya tatu ni Jaba Pool Klabu ambao walijinyakulia fedha
taslimu Shilingi 250,000/= na nafasi ya nne ilichukuliwa na klabu ya JBS ambao
walizawadiwa fedha taslimu Shilingi 100,000/=.
Upande wa
mchezaji mmoja mmoja wanaume Salum Yusuf alifanikiwa kutwaa ubingwa wa mkoa na
kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi 400,000/= pamoja na tiketi ya kuwakilisha
Mkoa wa Kinondoni kwenye fainali za Taifa upande wa wanaume na nafasi ya pili
ilichukuliwa na Mohamed Idd ambaye alizawadiwa Shilingi 250,000/=
Mchezaji
mmoja mmoja Wanawake, Grace Thomas alifanikiwa kutwaa ubingwa huo na kuzawadiwa
fedha taslimu Shilingi 300,000/= pamoja na kuwakilisha mkoa katika fainali za
kitaifa upande wa wanawake.Nafasi ya pili ilichukuliwa naCecilia Kileo ambaye
alizawadiwa fedha taslimu Shilingi 200,000/=.
Fainali za
kitaifa za 2014 za “Safari National Pool Competion” zinatarajiwa kufanyika
Moshi Mkoani Kilimanjaro kwa kushilikisha Mikoa 17 ambayo ni
Tabora,Shinyanga,Dodoma
Mbeya,Iringa,Morogoro,Mwanza,Kagera,Manyara,Arusha,Tanga,Pwani,Ilala,Lindi,Temeke,Kinondoni
na wenyeji wa mashindano kwa mwaka huu mkoa wa Kilimanjaro.
|
Post a Comment