MIKAKATI YA KUBORESHA SHULE ZA JUMUIYA YA WAZAZI YAANDALIWA
Katibu wa CCM wilaya ya muheza mkoani Tanga, Josephine
Thomasi (aliyesimama) akimkaribisha Mwenyekiti wa Jumuia ya Wazazi mkoani humo,
Dk.Edmund Mndolwa, wakati wa ziara yake ya kutoa shukrani kwa kumchagua na pia
kueleza uhai wa jumuia hiyo. Kikao hicho kilichofanyika katika ofisi za CCM
wilayani humo, kilihudhuriwa na viongozi mbalimbali ya jumuia hiyo kuanzia kata
na wilaya.
Mwenyekiti
wa Jumuia ya wazazi mkoa wa Tanga, Dk. Edmund Mndolwa, wa nne kulia,
akiwa na baadhi ya viongozi wa bodi ya Shule ya Sekondari Shemvua
iliyoko wilaya ya Lushoto mkoani Tanga, wanafunzi wa shule hiyo na
viongozi wa jumuia hiyo mkoani Tanga. shule hiyo inamilikiwa na jumuia
ya wazazi.
TANGA, Tanzania
MWENYEKITI
wa Jumuia ya wazazi mkoani Tanga, Dk. Edmund Mndolwa, amesema kuna mikakati ya
haraka ya kuboresha shule za Jumuia hiyo ili ziweze kutoa elimu bora.
Alisema
shule za jumuia ya wazazi zilikuwa kimbilio la wazazi na Watanzania kwa jumla,
lakini kwa sasa zinakabiliwa na soko la ushindani kutokana na shule nyingi za
kata na binafsi.
Akizungumza
katika ziara ya kutoa shukrani katika mkoa wa Tanga kwa kuchaguliwa kuwa
mwenyekiti wa jumuia hiyo, Dk. Mndolwa alisema shule za wazazi zote nchini
zinakabiliwa na uhaba wa walimu, vitendea kazi na vitabu.
Alieleza
kuwa shule hizo zimekuwa na tatizo la mfumo wa uendeshaji wake, kitu
kinachochangia kujiendesha kiholela na wakuu wa shule kuzichukulia kama zao.
“Tunatakiwa
kubadilika na kuzirejesha shule zetu katika hali yake ya zamani. Kwa kufanya
hivyo, tutawafanya Watanzania waendelee kuzikimbilia shule hizo ambazo zilikuwa
mkombozi kwao,
“Tushirikiane
kuanzia wazazi kwa kulipa ada ili walimu wapate mishahara mizuri na wakipata mishahara
mizuri watafundisha kwa ari na moyo, hivyo hata watoto wetu watapata elimu
nzuri,”alieleza Dk. Mndolwa.
Dk.
Mndolwa alisema kuwa mkoa wa Tanga una shule za wazazi sita huku nchi nzima
kukiwa na shule za wazazi 71.
Aidha,
akizungumza katika wilaya za Mkinga, Muheza na Pangani, Dk. Mndolwa aliwataka viongozi wa
jumuia hiyo kuwa watumishi wa watu kwa kwenda kusikiliza kero zao katika ngazi
za chini badala ya kujifungia ofsini.
Vilevile,
aliwataka viongozi hao kuachana na dhuluma kwa wanachama wanapokuwa wanaomba
nafasi ya uongozi, kwani kwa kuendeleza dhuluma kunachangia kupunguza nguvu ya
chama.
“Unakuta
mwanachama anakubalika na wananchi lakini kwa sababu ya chuki na dhuluma
anapewa mtu mwingine ambaye hakuongoza kura za maoni, hali ambayo hujenga chuki
kwa wanachama na kuamua kuwapigia kura wapinzania,
“Ukiangalia,
nafasi nyingi tulizopoteza katika ngazi mbalimbali kuanzia wenyeviti wa
serikali za mitaa, udiwani na ubunge, nafasi nyingi zimetokana na dhuluma, na
waliowachagua wapinzania ni wanaCCM wenyewe kwa sababu ya kuchukizwa kwa mtu
waliyempenda kutorudishwa jina lake,”alieleza.
Post a Comment