ad

ad

MAMIA WAJITOKEZA MKUTANO WA KUDAI MCHAKATO HURU WA KATIBA MPYA


Wafuasi wa CUF wakifuatilia mkutano huo.

Umati wa watu waliojitokeza katika mkutano wa hadhara wa kuwahamasisha wananchi kuungana na kudai mchakato huru wa katiba mpya unaoshirikisha wananchi wote uliofanyika leo kwenye viwanja vya Jangwani jijini Dar es Salaam. (Picha na Francis Dande)
 Umati uliojitokeza leo.
 Tunafuatilia kwa makini mkutano.....

 
 Tundu Lissu.
 Mabele Marando.
Mbunge wa Ubungo (Chadema),  John Mnyika.
Mwenyekiti wa NCCR-Mageuzi,  James Mbatia.
 Askofu Kakobe.
 Mhadhiri wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Azaveli Lwaitama. 

DKT. SLAA ATUA WASHNGTON DC KUTETA NA WANA DMV



Picha ya Juu na chini ni Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Wilboard Slaa pamoja na mchumba wake Josephine Mshumbuzi wakipokelewa na Makamanda wa CHADEMA DMV wakiongozwa na Mwenyekiti Kalley Pandukizi na Katibu wake Liberatus Mwang'ombe alipowasili kwenye uwanja wa ndege wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia. Dr. Slaa leo Jumapili Sept 22, 2013 atafanya mkutano na wana DMV kwenye ukumbi wa Marage  uliopo 1401 University Blvd, Hyattsville, MD 20783 kuanzia saa 7 mchana (1pm)


Kutoka kushoto ni Mweka Hazina wa CHADEMA DMV Ludigo Muhagama, Mwenyekiti wa CHADEMA DMV, Bwn. Kalley Pandukizi, Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt Wilboard Slaa, Bi. Josephine Mshumbuzi (mchumba wa Dkt Slaa), Katibu Mkuu baraza la wanawake CHADEMA DMV, Bi. Baybe Mgaza, Katibu Mkuu na afisa habari wa CHADEMA DMV, Bwn. Liberatus Mwang'ombe, Katibu Mkuu baraza la wazee CHADEMA DMV Elius Mshana, Julia Nyerere na Helena Nyerere katika picha ya pamoja na wageni wao. KUSOMA ZAIDI BOFYA READ MORE

Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Mwenyekiti wa CHADEMA DMV, Bwn. Kalley Pandukizi.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu na Afisa Habari wa CHADEMA DMV Bwn. Liberatus Mwang'ombe.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Katibu Mkuu wa Baraza la kina mama CHADEMA DMV Bi Baybe Mgaza.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Katibu wa wazee CHADEMA DMV, Bwn. Elius Mshana.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na mweka hazina wa CHADEMA DMV, Ludigo Muhagama.
Katibu Mkuu wa CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa katika picha ya pamoja na Julia Nyerere (kushoto) na Helena Nyerere.
Kutoka kushoto ni Mwenyekiti CHDEMA DMV, Bwn. Kalley Pandukizi, Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa, Bi. Josephine Mshumbuzi na Katibu Mkuu na Afisa habari wa CHADEMA DMV, Bwn. Liberatus Mwang'ombe katika picha ya pamoja.
Kutoka kushoto ni Katibu Mkuu wa wananwake CHADEMA DMV, Katibu Mkuu CHADEMA, Dkt. Wilboard Slaa na Bi. Josephine Mshumbuzi.
Makamanda wakisubiri kumpokea Katibu mkuu wa CHADEMA Dkt. Wilboard Slaa alipokua akiwasili leo Jumamosi Sept 21, 2013 kwenye uwanja wa kimataifa wa Dulles uliopo Sterling, Virginia.
Picha zote kwa hisani ya Vijimambo Blog

SIMBA YASHIKWA TAIFA, TAMBWE BALAA


Mshambuliaji wa Simba, Amis Tambwe akiwanyamazisha mashabiki wa Yanga baada ya kuifungia timu yake bao la pili

VINARA wa Ligi Kuu Tanzania Bara, Simba leo wamepunguza kasi baada ya kulazimishwa sare ya mabao 2-2 na Mbeya City katika mchezo wa kuvutia uliochezwa kwenye Uwanja wa Taifa, Dar es Salaam.

Pamoja na Simba kulazimishwa sare hiyo lakini Mshambuliaji wake, Amis Tambwe ameendeleza makali yake baada ya kluifungia timu yake mabao yote mawili na kufanya azidi kukaa kileleni mwa orodha ya wafungaji wa mabao katika ligi hiyo kwa kufikisha mabao sita baada ya kufunga mabao manne katika mchezo uliopita dhidi ya Mgambo Shooting.

Mbeya City ambayo hii ni sare yao ya tatu mfululizo, ambapo sare yao ya kwanza walianza na Yanga jijini Mbeya, wakafuatia sare na Mtibwa katikati ya wiki, waliamua kutoka usingizi na kupata mabao yake ya kusawazisha kupitia kwa Paul Nonga na Richard Peter.
 Haruna Chanongo akiwa kibaruani katika mchezo huo
Aliyekuwa mshambuliaji wa Simba, Emmanuel Okwi alikuwepo uwanjani, akiwapungia mashabiki wa timu hiyo

MATOKEO YA MICHEZO MINGINE YA LIGI 

MGAMBO 1-1 RHINO 
KAGERA 3-0 ASHANTI
PRISONS 1-1 MTIBWA 

MICHEZO YA LEO YA LIGI 


JKT RUVU         vs    JKT OLJORO            CHAMANZI
AZAM                vs    YANGA                     TAIFA
COASTAL          vs    RUVU                        MKWAKWANI

No comments