MWANAFUNZI IFM KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI, NI WENDE LWENDO ALIYEKUFA MWANAFUNZI IFM KUZIKWA KESHO MAKABURI YA KINONDONI, NI WENDE LWENDO ALIYEKUFA MAJI
MAZISHI ya Mwanafunzi na Rais wa Taasisi ya wanafunzi AIESEC- IFM, Wende Lwendo wa Mwaka wa Kwanza Uhandisi Kompyuta wa Chuo cha Usimamizi wa Fedha (IFM) aliyefariki juzi kwa kufa maji baharini yanafanyika kesho.
Wende , alifariki katika ufukwe wa bahari ya Hindi eneo la Kipepeo Kigamboni jijini Dar es Salaam akiogelea na wenzake watatu majira ya jioni baada ya kumaliza mitihani yao ya kufunga mwaka wa masomo.
Kaka wa marehemu, Sammy Lwendo ameiambia Father Kidevu Blog leo kuwa marehemu anataraji kuzikwa kesho alasiri katika makaburi ya Kinondoni na mipango yote ya mazishi inaendelea vizuri.
Lwendo amesema kuwa mipango ya mazishi ilikuwa ikisubiri wazazi wa marehu ambao waliwasili juzi usiku wakitoakea mkoani Arusha na kutaarifu ndugu kuwa mazishi yatafanyika Dar es Salaam.

Post a Comment