MIKOA 10 YAANZA VYEMA KUSAKA MABINGWA WA KUWAKILISHA MIKOA SAFARI POOL
Jamali
Ngoma wa timu ya Flamingo Klab akicheza dhidi ya timu ya Yakwetu Klab wakati wa ufunguzi wa
mashindano ya Pool Taifa ngazi ya Mkoa,Mkoa wa Pwani yaliyofanyika kwenye Baa ya Kontena
Kibaha Maili moja, Mashindano haya yanadhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kupitia Bia ya Safari Lager yakijulikana kwa Safari National Pool Competition 2013.
Syakyala Mwansasu wa timu ya
Flamingo akichecheza wakati ufunguzi huo.
Yakob Msando wa timu ya Kontena
akimalizia mpira mweusi wakati wa ufunguzi wa mashindano hayo dhidi ya Klabu ya Kiluvya B.
Na mwandishi wetu,Kibaha
Mikoa iliyoanza mashindano ya Safari Pool Taifa wiki hii ni Pwani,Lindi,Mwanza Mara,Arusha ,Tanga ,Manyara,Temeke ,Ilala na Kinondoni.
Mikoa ambayo tunatarajia itapata mabingwa watakaowakilisha mikoa hii ambao ni vilabu ni Pwani,Lindi Mwanza,Mara,Arusha,Tanda,na manyara ambapo mashindano haya yanatarajiwa kumalizika mwishoni mwa wiki hii jumapili.
Mikoa ambayo tayari ilmeshapata mabingwa watakao wakilisha mikoa yao katika mashindano ya kitaifa Mkoani Morogoro Augusti 19 mpka 22 ni Shinyanga,Tabora,Kagera na Kilimanjaro.
Baada ya hapa kutakuwa na mapumziko ya mwezi mmoja kwa mfungo wa Ramadhani na baadae mashindano yataendelea kwa mikoa iliyobaki
Baada ya hapa kutakuwa na mapumziko ya mwezi mmoja kwa mfungo wa Ramadhani na baadae mashindano yataendelea kwa mikoa iliyobaki
Post a Comment