AMINI KAIBUKA NA 'WHY MIMI'
Pia alisema anatanguliza audio kwa lengo la kuwaweka sawa mashabiki wake, ikiwa ni pamoja na kuwatayarisha kwa ajili ya kazi zake nyingine ambazo zinakuja hivi karibuni.
MKALI wa muziki wa
kizazi kipya nchini, Amini Mwinyimkuu ‘Amini’, anatarajiwa kuachia kibao chake
kipya kinachokwenda kwa jina la ‘Why Mimi’.
Amini, amesema katika kazi hiyo ameshirikiana vyema na msanii Barnaba Elias
iBarnaba Boy’ anaamini kazi hiyo itapokelewa vyema na kushika chati katika
tasnia ya muziki huo kutokana na uwepo wa mwanamuziki huyo anae bamba katika
tasnia hiyo.
Akizungumza jijini Dar es Salaam, Amini alisema yupo
katika hatua za mwisho za uandaaji wa kibao hicho, ambacho amekitengeneza
katika Studio ya Surround Records chini ya mtayarishaji wake maarufu, Emma The
Boy.
“Naomba mashabiki wangu wakae mkao wa kula kwa ajili ya kukipokea kibao hiki,
ambacho naamini kitaelimisha na kuburudisha jamii inayotuzunguka,” alisema
Amini.
Post a Comment