ad

ad

RC Arusha mgeni rasmi fainali Nyama Choma

Jaji Mkuu wa mashindano ya Safari Lager Nyama Choma, Douglas Sakibu (kushoto) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu fainali za Safari Nyama Choma Mkoa wa Arusha na Moshi mwishoni mwa wiki.Kutoka Kulia ni Meneja Mauzo wa Kanda, Kitio Wilderson,Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo na Meneja wa Kanda ya Kaskazini TBL, Kisiro Msangi.
Na Mwandishi Wetu, Arusha
MKUU wa Mkoa wa Arusha, Magesa Mulongo, anatarajiwa kuwa mgeni rasmi katika fainali za kunyoma nyma, zinazodhaminiwa na Kampuni ya Bia Tanzania (TBL), kupitia bia ya Safari Lager, itakayofanyika Jumamosi kwenye viwanja vya General Tyre.
Akizungumza mjini hapa, Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo, ni fahari kubwa kwa TBL kupitia Safari Lager kufanikisha shindano hilo mkoani hapa kabla ya kuhamia mikoa mingine.
Alizitaja baa zitakazochuana Jumamosi kuwa ni Blue Line Park, VIP Lounge, QX Pub, Royal Stop Over na Rombo Deluxe, ambapo bendi ya Yekete, pamoja na kikundi cha sarakasi vitatoa burudani katika fainali hiyo.
“Fainali ya Safari Lager Nyama Choma Mkoa wa Arusha itafanyika Jumamosi na hizo baa tano ndio zitakazochuana, tulianza kwa kuwataka watu wapige kura kupendekeza baa zinazofaa kuingia katika shindano.
“Tunajua watu huwa wanakwenda katika baa na kula nyama, hivyo tukaona ni vema tuanzishe mashindano haya ili walaji nyama choma wapate nyama bora,” alisema Shelukindo.
Kwa upande wake, Jaji Mkuu wa fainali hizo, Douglas Sakibu, alisema kabla ya shindano hilo, walitoa mafunzo kwa baa zote hizo juu ya mambo wanayopaswa kuzingatia katika uchomaji nyama.

Alisema watatumia vigezo kumpata mshindi ambavyo ni usafi wa nyama, vifaa na mazingira, maandalizi ya nyama kuanzia uchaguzi, uhifadhi wake na wa vifaa, uchomaji na upangaji nyama, ladha na ulaini wake, mazingira ya eneo, mtiririko wa maji na uhifadhi wa taka.
Mshindi wa kwanza atajinyakulia Sh 1, 000,000 na cheti, wa pili Sh 800,000 na cheti, wa tatu Sh 600,000 na cheti, wa nne Sh 400,000 na cheti, wakati mshindi wa tano atapata Sh 200,000 na cheti.

No comments