SAFARI LAGER YAZINDUA RASMI SHINDANO LA UCHOMAJI NYAMA KWA BAA BAA MBALIMBALI KWA MWAKA 2013.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo(kulia)
akikata nyama kuashilia uzinduzi wa shindano la Safari Lager Nyama Choma
linalotammbulika kwa jina la “Safari Lager Nyama Choma Competition
2013”lililozinduliwa TBL jijini Dar es Salaam.Kushoto ni Jaji Mkuu wa shindano
hilo, Douglass Sakibu.
Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar Shelukindo (katikati)
akizungumza na waandishi wa habari (hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa
shindano la Nyama Choma 2013 kwa Bar mbalimbali lijlikanalo kama ‘’Safari Lager
Nyama Choma Competition 2013” liliofanyika TBL jijini Dar es Salaam .Kulia ni
Jaji Mkuu wa shindano hilo, Douglass Sakibu na mratibu wa Shindano hilo, Peter
Zacharia.
KAMPUNI
ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imezindua rasmi
shindano lauchomaji nyama kwa baa mbalimbali lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition
2013”.
Shindano hili linalofanyika kila
mwaka, linafanyika mwaka huu kwa mara ya sita mfululizo na litashirikisha mikoa
ya Mbeya, Kilimanjaro, Arusha, Mwanza na Dar Es Salaam. Tangu lilipoanzishwa
mwaka 2008, shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya
Safari Lager kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha
zinaibuka na ushindi katika mkoa waliopo. Kwa mwaka huu walaji wa nyama choma
watatakiwa kupigia baa zao kura kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutumia simu
za mkononi kwenda namba0763 514 514.
Ujumbe huu utatozwa gharama za kawaida za kutuma ujumbe, hakutakuwa na makato
ya ziada kwa mitandao ya simu. Baa tano zitakazopata kura nyingi zaidi
zitachuana kwa kuchoma nyama katika tamasha la wazi litakaloandaliwa katika
mikoa yote, washindi watapata zawadi mbalimbali ikiwamo fedha taslimu. Zaidi ya
shilingi milioni ishirini na sita zitatolewa kama zawadi kwa washindi mwaka
huu.
Akizungumza na waandishi wa habari
jijini Dar Es Salaam, meneja wa bia ya Safari Lager bwana Oscar Shelukindo
alisema kwamba, “Lengo kuu la shindano la Safari
Lager Nyama Choma ni kuongeza hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama
choma ili kwa pamoja waweze kufahamu viwango bora katika uchomaji na utayarishaji
wa nyama choma. Tunahakikisha wachoma nyama katika baa za mikoa yote
inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa kutosha katika fani hii ili kumpa
mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama choma. Tumezingatia maombi ya
washiriki mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya
uchomaji nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache
zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Bwana Shelukindo
aliendelea kufafanua kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha
nyama choma za aina tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.
Kiongozi wa jopo la majaji ambao ni
wataalamu maarufu nchini katika tasnia hii, bwana Douglass Sakibu alielezea
kwamba majaji wataangalia kwa makini sana vigezo mbalimbali katika utayarishaji
wa nyama choma. Alitaja baadhi ya vigezo hivyo kwamba ni usafi, vifaa vya
kufanyia kazi, joto maalum la uchomaji nyama nk. Bwana Sakibu aliendelea kusema
kwamba, “Tunawaomba bar zote kujitokeza katika semina ya utangulizi
tutakayofanya katika mikoa yote inayoshiriki, Katika semina hii tutakumbushana
mambo muhimu ya kuzingatia ili kumpa mteja nyama choma bora zaidi, muda wote
anapoihitaji”.
Naye bwana Peter Zacharia, wa
kampuni ya Integrated Communications inayoratibu shindano la Safari Lager Nyama
Choma alisema, “Tunaomba wachoma nyama kujitokeza kwenye semina hizi, mafunzo
yatatolewa bure. Seminar kwa baa za wilaya ya Temeke itafanyika Imasco Bar
uwanja wa Taifa Jumatatu tarehe 11 February. Baa za wilaya ya Ilala seminar
itafanyika Jumanne tarehe 12 February katika baa ya Beriego Ilala Bungoni. Kwa
wilaya ya Kinondoni semina itafanyika Jumatano tarehe 13 February katika baa ya
Meeda Sinza”. Bwana Peter alitaja pia tarehe za semina za mikoani kama
ifuatavyo; Baa za mkoa wa Mbeya, Ijumaa tarehe 8 February, baa za mkoa wa
Mwanza Ijumaa tarehe 22 February, baa za mkoa wa Arusha Jumatano tarehe 27
February na baa za mkoa wa Kilimanjaro Alhamisi tarehe 28 February.
Bwana Shelukindo alimaliza kwa kusema
kwamba, “Safari Lagertutaendeleakujitahidikuhakikishawatejawetuwanapatahuduma
bora yanyamachoma pale wanapoihitaji. Tunawaombasanawashirikikutumiavizurielimunauzoefuwanaopatailikuongezauborawautayarishajiwanyamachomakwawatejawetu.
MashindanohayayaSafari Lager NyamaChomayatakosamaanasahihiendapowachomanyamawatakuwawanashirikikwalengo
la kujipatiamanufaabinafsinakusahauyaleyotewaliyojifunzahadimwakamwingine”.Shindalo
la mwakahuulinaongozwanakibwagizo…. Bila
Safari Lager, NyamaChomahaijakamilika!.
Post a Comment