Mwanamichezo Oscar Pistorius mikononi mwa Polisi kwa mauaji Afrika Kusini!
Mwanariadha
mlemavu Oscar Pistorius wa Afrika Kusini ashikiliwa na Polisi!kwa shutuma za kumuua Mpenzi wake !
WAKATI wengine wanasherekea siku ya wapendanao duniani ! lakini kwa
mwanamichezo
Oscar Pistorius imekua kinyume ! badala ya furaha ni msiba!
Asubuhi na mapema alhamisi 14/02/2013 huko Pretoria, Afrika kusini Polisi
walitia mkononi mwanamichezo nyota
aliyejipatia umarufu katika michezo ya Olympic Bw.Oscar Pistorius
(26),ametiwa nguvuni
ana polisi wa nchi hiyo kwa madai ya kumuua mpenzi wake model Reeva
Steenkamp kwa kumpiga risasi!
Inasemekana alhamisi 14/02/2013 asubuhi milio ya risasi ilisikika nyumbani
kwa mwanamichezo huyo mjini Pretoria na polisi walipofika
walimkuta mpenzi wa mwanamichezo huyo Bi. Reeva Steenkamp (30) ambae pia ni
model ameshauwawa.
Polisi wa Afrika kusini wanategemea kumfikisha mahakamani bw.Oscar
Pistorius (26) kwa mashtaka ya mauaji
siku ya ijumaa ya 15/02/2013.
Post a Comment