Zaidi ya wanakijiji 600 wapewa huduma ya afya Monduli.
Dk.Song Gmhwa(kulia) raia wa Korea akimwangalia Bibi wa
kimasai, Naniai Poranda, macho kwa kutumia kifaa maalum ambayo yanamatatizo ya
kuona wakati wa huduma ya afya ya kujitolea ya wafanyakazi wa Samsung Medical
Center na Sumsung Electronics iliyofanyika katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya
ya Monduli Mkoani Arusha jana.Zaidi ya watu 600 walipewa matibabu.
Na Mwandishi Wetu-Arusha
Wanakijiji zaidi ya 6000 wanaoishi
katika Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha wamepata huduma ya afya ikiwa ni pamoja
na upimaji wa magonjwa mbalimbali sanjari na utowaji wa madawa.
Zoezi hilo ambalo linaendeshwa na
Kampuni ya Samsung kupitia wafanyakazi wake Samsung Medical Center na Samsung
electronics kwa kujitolea wakishirikiana na shirika la Chakula kwa ajili ya
Majanga la Korea(KHFI) wanaendesha zoezi
la upimaji wa magonjwa mbalimbali pamoja na utowaji wa madawa kwa wanakijiji
hao.
Meneja wa Kampuni ya Samsung kwa
Afrika mashariki Bw.Makunga Mugo nalisema kuwa wafanyakazi kutoka katika
kampuni hiyo wanajitolea katika kuwasaidia wananchi mbalimba wenye mahitaji kwa
Afrika nzima na sasa wako Tanzania Mkoani Arusha.
Alisema kuwa wamejikita zaidi kwa
vijana huku akidai kuwa wao ndio nguvu kazi katika kila nchi kwani wanaamini
wakimuwezesha kijana wamewezesha jamii nzima inayomzunguka.
Naye diwani wa kata ya Elmorijo
Bw.Bariki Sumuni alisema kuwa anatoa shukrani kwa wafadhi hao kwa kuwa
wamejaribu kuokoa maisha ya wazee,wamama,vijana na watoto kwa kutoa huduma ya
vipimo pamoja na utowaji wa madawa bure jambo ambalo limekuwa ni changamoto
kubwa katika kijiji hicho.
Alisema kuwa huduma ya Afya ipo
umbali kwa kilometa 12 hadi kufikia katika zahanati ya kijiji hali ambayo
imekuwa ikiwapa shida hasa kwa kinamama wajawazito wakati wa cliniki na wakati
wa kujifungua.
Aidha alisema kuwa changamoto
nyingine ni pamoja na uhaba wa upatikanaji wa maji kijiji hapo kutokana na eneo
hilo kuwa katika muinuko wa juu kama panavyojulikana kwa jina la Monduli juu.
“Kampuni ya Samsung imetusaidia sana
hapa kijijini hata imetujengea shule na pia nimezungumza nao wamenihaidi kuwa
watajenga zahanati hapa kwakuwa tayari kunampango wa kuwa na kijiji kipya
kutokana na ongezeko la watu”alisema Sumuni.
Kwa upande wake mfanyakazi KHFI na Korea
charch mission Bw.Daniel Vayani alisema
kuwa wametenga kiasi cha shilingi milioni 100 kwaajili ya ukarabati wa shule pamoja
na kuwasomesha bure watoto wanaoshi katika mazingira magumu.
Alisema kuwa changamoto iliyopo kwa
sasa ni pamoja na kuwepo kwa muamko mdogo wa elimu katika mila,watoto kukatisha
masomo
Mmoja wa wagonjwa aliyepatiwa
matibabu ya bure katika zoezi hilo Bi.Maria Devid (60)alisema kuwa yeye
alifanyiwa upimaji katika baadhi ya mwili wake ambapo alikuwa akisumbuliwa na
maumivu ya kichwa,macho na kutosikia vizuri
“Kweli nawashukuru sana hawa
wafadhili Mungu awabariki kwa kuja kutupa hii huduma ya bure ,zahanati yetu ya
kijiji ipo mbali hivyo leo tumepata fursa nzuri sana”alisema
Katika zoezi hilo pia upimaji wa
magonjwa mbalimbali unafanyika na upimaji huo unawashirikisha
wazee,vijana,wanafunzi pamoja na watoto wadogo ambapo zoezi hilo litadumu kwa
siku mbili.
Dk.Song Gmhwa(kulia) raia wa Korea akimwangalia Bibi wa
kimasai, Naniai Poranda, kinywa kwa kutumia kifaa maalum wakati wa huduma ya afya ya kujitolea ya
wafanyakazi wa Samsung Medical Center na Sumsung Electronics iliyofanyika
katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya ya Monduli Mkoani Arusha jana.Zaidi ya watu
600 walipewa matibabu
Dk. Seung Woo Park(kulia) raia wa Korea akimpima Bibi wa kimasai,Ngaisi Sumuni wakati
wa huduma ya afya ya kujitolea ya wafanyakazi wa Samsung Medical Center na
Sumsung Electronics iliyofanyika katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya ya Monduli
Mkoani Arusha jana.Zaidi ya watu 600 walipewa matibabu.
Dk.Moon Eunmi (kushoto) raia wa Korea akimwelekeza Mama wa
kimasai,Nariku Ngera namna ya kutumia dawa kwa kumpa Mtoto wakati wa huduma ya
afya ya kujitolea ya wafanyakazi wa Samsung Medical Center na Sumsung
Electronics iliyofanyika katika kijiji cha Elmorijo, Wilaya ya Monduli Mkoani
Arusha jana.Zaidi ya watu 600 walipewa matibabu
Post a Comment