ad

ad

JIJINI


Na Kambi Mbwana
ONYESHO la mavazi la Lady in Red linalotarajiwa kufanyika Februari 11 limeendelea kupata wadhamini baada ya kampuni ya matangazo ya luninga barabarani ya Nova Media kudhamini ‘shoo’ hiyo.
Akizungumza na Papaso la Burudani mwandaaji wa onyesho hilo, Asia Idarous alisema kampuni hiyo imedhamini onyesho hilo na itakuwa ikirusha matangazo kupitia mabango yao yaliyopo barabarani.
“Tunashukuru tumepata wadhamini wengine ambao watatusaidia katika matangazo hasa yale ya barabarani, hii ni dalili nzuri kwetu na inaonyesha kuwa tutafanikiwa katika lengo letu,” alisema Asia.
Onyesho hilo ambalo litapambwa na warembo wa kisura na wasanii wa muziki wa bongo fleva Baby Madaha, Chidi Benz pamoja na bendi ya Bablom Trio, asilimia 10 ya pato litakalopatikana litasaidia waathirika wa dawa za kulevya wa kituo cha Drugs Free kilichopo Visiwani Zanzibar.
Onyesho hilo ambalo ni la sita kufanyika na la 80 katika jumla ya maonyesho yake yote aliyofanya ndani na nje ya nchi litafanyika katika Ukumbi wa Hoteli ya Movenpick




Na Kambi Mbwana
UONGOZI wa TOT Plus Taarab umetamba kufanya uzinduzi wa albamu yao kwa mapinduzi makubwa, ili kuonyesha makali yao katika tasnia ya muziki huo hapa nchini.

Uzinduzi wa albamu ya TOT inayojulikana kama ‘Top in Town’, ikiwa chini ya malkia wa mipasho hapa nchini, Khadija Omary Kopa, unatarajiwa kufanyika Februari 14, katika Ukumbi wa Travertine, Magomeni, jijini Dar es Salaam.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, Katibu wa Tanzania One Theatre inayomiliki bendi hiyo, Gasper Tumaini, alisema kwamba wapo kwenye maandalizi makubwa ili kufanikisha uzinduzi wa albamu hiyo ya Top in Town.

Alisema kwamba kila kitu kinaendelea vizuri katika kuhakikisha kwamba mambo yanakuwa mazuri, kutokana na mipango wanayoendelea kuifanya.

“Nia ni kufanya uzinduzi wa kutisha na kuonyesha makali yetu katika kona ya muziki wa taarabu hapa nchini, hivyo naamini kwamba wadau na mashabiki wa muziki wa taarabu watapa kitu kizuri kutoka kwa waimbaji wetu.

“Sisi kama uongozi wa TOT Plus Taarab, tunashirikiana kwa kiasi kikubwa na wanamuziki wetu, ukizingatia kwamba tunahamu ya kuona bendi inafanya mambo mazuri katika uzinduzi huo,” alisema Tumaini.

Mbali na bendi hiyo, pia Khalid Mohamed akiwa chini ya Top Band, wanatarajiwa kuusindikiza uzinduzi huo wa Jumatatu, huku ukisubiriwa kwa hamu na mashabiki wao.

No comments