ad

ad

JIJINI

Ngumi Ilala kuanza Ijumaa

NA MWANDISHI WETU

MASHINDANO ya klabu bingwa ya ngumi za ridhaa mkoa wa Ilala yanatarajia kuanza Ijumaa katika ukumbi wa CCM Amana.

Akizungumza jana jijini Dar es Salaam, msemaji wa mashindano hayo Lemmy Ngaboh, alisema baada ya kampuni ya Kinyogoli Foundation of Tanzania kudhamini mashindano hayo sasa maandalizi yamekamilika.

Ngaboh alizitaja timu zilizodhibitisha kushiriki mashindano hayo kuwa ni Magereza, Ashanti, Chanika, Gongolamboto, Kariakoo, Vingunguti na Amana.

Lyon kubadilisha jina

NA ZAITUNI KIBWANA

TIMU ya soka ya African Lyon, Januari 10, itafanya hafla ya uzinduzi wa jina jipya. Uzinduzi huo utafanyika siku tano kabla ya kuanza kwa Ligi Kuu ya soka Tanzania Bara inayotarajia kuanza Januari 15 katika vituo mbalimbali.

Timu hiyo imebadilishwa jina baada ya kununuliwa na Mkurugenzi wa Kampuni ya RBP &Industrial Technology Limited ambaye pia ni mlezi wa timu ya Taifa ya wanawake

(Twiga Stars) Rahma Al Kharoosi.

Akizungumza na Bingwa jana, kocha mkuu wa timu hiyo Jumanne Chale alisema lengo la kufanya uzinduzi huo ni kuwatambulisha Watanzania ujio wa timu yao mpya kwa sasa.

Maugo hakujiandaa

NA ZAITUNI KIBWANA

MWENYEKITI wa waamuzi wa mchezo wa ngumi nchini, Ally Bakari ‘Champion’ alisema kuwa bondia Mada Maugo alipigwa kutokana na kutojiandaa vya kutosha katika pambano hilo.

Akizungumza Dar es Salaam jana Champion alisema kuwa kichapo alichokipata Maugo kilikuwa halali na kwamba waamuzi waliamua kwa haki.

Pambano hilo lilifanyika katika Ukumbi wa PTA jijini Dar es Saalam, ambapo Cheka aliibuka na ushindi dhidi ya mpinzani wake kwa pointi mbili ambazo zilitolewa na majaji watatu ambapo jaji wa kwanza alitowa 79- 79, 79- 78, 79- 78.

No comments