Kili Stars hureee robo fainali
Na Rachel Mwilligwa
NI Shujaa Nurdin Bakari, ndivyo unavyoweza kuisimulia timu ya Taifa ya Kilimanjaro Stars kufanikiwa kutinga hatua ya robo fainali ya michuano ya Kombe la CECAFA inayoendelea jijini.
Mabao yake mawili ya vichwa vya uhakika, yalitosha kabisa kuihakikishia Kili Stars kutinga hatua hiyo muhimu iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki.
Hiyo ni kutokana na Kili Stars kupoteza mchezo wake wa ufunguzi dhidi ya Zambia baada ya kukubali kipigo cha bao 1-0 kabla ya kuibuka na ushindi wa mabao 3-0 dhidi ya Somalia.
Ikicheza kwa kujiamini huku ikishangiliwa na umati wa mashabiki wa soka nchini waliofurika kuishangilia, Stars ilijipatia mabao hayo kupitia kwa Nurdin Bakari ambaye anaweza kuitwa shujaa wa kweli wa mchezo huo.
Nurdin aliiandikia Kili Stars bao hilo safi la kichwa akiunganisha krosi ya Mrisho Ngassa, kichwa kilichomshinda mlinda mlango wa Burundi Niyonkuru Vladimir.
Ki ukweli katika pambano hilo ambalo matokeo yake yalikuwa na umuhimu mkubwa kwa Kili Stars, wawakilishi hao wa Tanzania Bara, walionesha uwezo mkubwa hasa walipotawala vema kipindi cha kwanza.
Sasa Kili imetimiza kiu ya Watanzania kwa kutinga hatua hiyo ya robo fainali, ikiwa ni harakati za kutaka kulibakiza hilo nyumbani.
Kwa matokeo hayo, Kili Stars imeingia robo fainali pamoja na vinara wa kundi lake (Kundi A) Zambia, ambayo inaongoza kwa pointi tisa huku Kili ikiwa na pointi sita.
Akizungumza na waandishi wa habari baada ya mchezo huo, Kocha Mkuu wa Kili Stars, Jan Poulsen alisema amefurahishwa na kiwango kilichooneshwa na wachezaji wake.
“Nimefurahi kwa ushindi huu, timu imecheza vizuri na wachezaji wamerekebisha makosa yaliyojitokeza katika mchezo wetu wa ufunguzi dhidi ya Zambia Jumamosi (Novemba 27),” alisema Poulsen.
Stars: Juma Kaseja, Kelvin Yondan, Idrisa Rajabu, Shadrack Nsajigwa, Mohamed Banka, Henry Joseph, Nurdin Bakari, Stephano Mwasika na Juma Nyosso.
Sub: Shaaban Kado, Erasto Nyoni, Ramadhan Shamte, Salum Machaku, Jabir Aziz, Gaudence Mwaikimba na John Bocco.
Michuano hiyo itaendelea leo kwa mabingwa watetezi timu ya Uganda ‘The Cranes’kushuka dimbani kumenyana na Kenya ambao wametangaza kujitoa wakati Ivory Coast wao watapepetana na Sudan.
XxxxxxxxMWISHO
……….Nurdin Shujaa wa kweli
Na Mwandishi Wetu
MCHEZAJI wa Kilimanjaro Stars, Nurdin Bakari jana alionesha kuwa shujaa wa ukweli baada ya kuipeleka timu hiyo hatua ya robo fainali ya michuano ya CECAFA inayoendelea jijini.
Wakizungumza na Mtanzania baada ya pambano hilo, baadhi ya mashabiki waliofurika uwanjani walifurahia ushindi huo huku wakimwagia sifa nyingi mchezaji Nurdin Bakari.
“Kwa kweli leo (jana) Nurdin amecheza vizuri sana na imeonekana wanaelewana vema na kuonana na Mrisho Ngassa ambaye amekuwa akimpelekea krosi safi zilizozaa matunda.
“Leo Kili Stars imenifurahisha mno maana nimekuja nikiwa sijui nitatoka kichwa chini au vipi, lakini aibu ya wenyeji kutolewa mapema imeondoka,” alisema shabiki huyo aliyejitambulisha kwa jina moja la Haji.
Kwa matokeo hayo, Kili Stars inatakiwa ifanye jitihada za ziada kuhakikisha inaendeleza vema kiwango ilichoonesha kwenye pambano hilo katika michezo yake ijayo kuanzia hatua hiyo ya robo fainali.
Kwa namna ilivyocheza jana, Stars inatakiwa kuwa makini kwenye michezo yake ijayo kwasababu haikuwa makini sana na kukosa nafasi nyingi za kufunga hivyo ilekebishe kosa hilo.
xxxxxxxMWISHO

Post a Comment