
Mratibu wa Bonanza la Vyuo Vikuu vya jijini Dar es Salaam (Intellectuals Grand Malt Bonanza 2010), Innocent Meleck (kushoto) akiwakaribisha waandishi wa habari kwenye mkutanao.

Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam (katikati) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Bonanza la Grand Malt la Vyuo Vikuu vya Dar es Salaam, linalotarajiwa kufanyika Novemba 20, kwenye viwanja vya Kampuni ya Sigara (TTC) Chang’ombe. Kulia ni Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kayumba Torokoko na Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu Huria, Lawrence Adam.

Akizungumza

Mratibu wa Bonanza la Vyuo Vikuu vya jijini Dar es Salaam (Intellectuals Grand Malt Bonanza 2010), Innocent Meleck (kushoto), akizungumza na waandishi wa habari kuhusu Bonanza hilo, linalotarajiwa kufanyika Jumamosi ya Novemba 20, kwenye viwanja vya Kampuni ya Sigara (TTC). Katikati ni Meneja wa Kinywaji cha Grand Malt, Consolata Adam na Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kayumba Torokoko.

Waziri wa Michezo wa Chuo Kikuu cha Dar es Salaam, Kayumba Torokoko akishukuru.
Post a Comment