ad

ad

ALIYEKUWA MSEMAJI WA TFF,KAIJAGE APIGWA CHINI.

Aliyekuwa Msemaji wa TFF,Florian Kaijage
Kaijage akizungumza na Juma Pinto

Rais wa TFF, Leodger Tenga (kulia) akizungumza na waandishi wa habari kuhusu kusimamishwa kwa Ofisa habari wa TFF, Floriani Kaijage kwa kutopiga nyimbo za Taifa wakati wa Mechi ya Taifa Stars na Morocco.Kushoto ni Mkurugenzi wa Ufundi Sunday Kayuni


Shirikisho la soka nchini TFF limemsimamisha kazi msemaji wa TFF KAIJAGE baada kushindwa kupiga nyimbo za taifa wakati wa mchezo wa kufuzu fainali za mataifa ya afrika kati ya morocco na tanzania.

Kabla ya kuanza kwa mchezo huo ambapo rais kikwete alikuwa mgeni rasmi baada ya kukagua timu na kuanza kusubiri nyimbo za taifa hakunakilichosikika zaidi wapenzi wa yanga wakaanza kuimba mungu ibariki yanga.

Mpaka sasa bado haijafahamika kwanini nyimbo hizo zilishindwa kupigwa ,kufuatia kitendo hicho TFF imeamua kumsimamisha kazi msemaji wa tff kaijage mpaka hapo uchunguzi utakapokamili.

Rais wa tff tenga amesema kwa kushirikiana na wizara ya habari utamadunia na michezo wanaunda kamati ambayo itachunguza chanzo cha tatizo hilo huku kaijage akiwa nje mpaka hapo uchunguzi utakapo kamalika.

Lakini katika hatua nyingine tenga amesema ndani ya mwezi mmoja tff inatarajia kutangaza nafasi mbili ya katibu wa tff na msemaji wa tff ili kuziba nafasi hizo haraka .

No comments