Meneja wa Sabuni
ya Omo, Upendo Mkusa(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya kwanza, Gift Obed
Ondara pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada
na Omo” inayoendelea katika Supermakert ya Shoppers Mikocheni.Droo ya kwanza
ilichezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermakertn ya kubwa tatu tofauti ambayo
ni Choppies,Game Mlimani City na Shoppers Mikocheni na washindi watatu
walijishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/= kila mmoja.
Meneja wa
Sabuni ya Omo, Upendo Mkusa(kushoto) akimkabidhi mwakilishi wa mshindi wa droo ya kwanza ambae ni,
Isabela Sango Luhanga pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada
na Omo” inayoendelea katika Supermarket ya Game Mlimani City.Droo ya kwanza
ilichezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarket ya Choppies,Game Mlimani City
na Shoppers Mikocheni na washindi watatu walijishindia pesa taslimu Shilingi
500,000/= kila mmoja.
|
Meneja wa
Sabuni ya Omo, Upendo Mkusa(kushoto) akimkabidhi mshindi wa droo ya kwanza, Muzdalifa
Hamadi Haji pesa taslimu Shilingi laki tano(500,000/=) aliyoshinda katika Promosheni ya “Tusua Ada
na Omo” inayoendelea katika Supermakert ya Choppies Mlimani City.Droo ya kwanza
ilichezeshwa mwishoni mwa wiki katika Supermarkert ya kubwa tatu tofauti ambayo
ni Choppies,Game Mlimani City na Shoppers Mikocheni, washindi watatu
walijishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/= kila mmoja.
WASHINDI
watatu kutoka katika maeneo tofauti ya jijini Dar es Salaam wamejishindia jumla
ya pesa taslimu Shilingi 1,500,000/= ikiwa ni shilingi 500,000/= kila mmoja
katika promosheni ya Tusua Ada na Omo inayoendelea katika Supermakert kubwa ya
Game, Choppies Mlimani City na Shoppers Mikocheni,Masaki na Mbezi.
Washindi hao
walipatikana mara baada ya kununua Omo na kuingia rasmi kwenye droo kubwa inayochezeshwa
katika Supermakert hizo.
Akizungumza
na Waandishi wa Habari Meneja wa Omo, Upendo Mkusa kwanza aliwapongeza washindi
wote watatu wa droo ya kwanza na kuwaomba kama wana watoto wanasoma pesa hizo
wakazilekeze katika kuwasaidia watoto wao katika sekta ya kuwaendeleza kielimu.
Kampuni ya
Unilever kupitia bidhaa yake ya Sabuni ya Omo wanatambua kama jamii ya
Watanzania imetoka katika kipindi cha Siku kuu ya Chrismass na Mwaka mpya hivyo
wakaona ni jambo jema kuungana na wanafamilia katika kipindi hiki cha watoto
kwenda shule kuchangia kwa namna moja ama nyingine kupitia promosheni hii.
Alisema
Upendo, katika Promosheni hii ya Tusua Ada na Omo jumla ya Shilingi milioni
sita (6,000 000/=) zitatolewa
kwa washindi 12 ikiwa kila mmoja atajishindia pesa taslimu Shilingi laki
tano(500,000/=).
Alisema
Upendu ushiriki uko wazi kwa kila mtu lakini lazima uwe na umri zaidi ya miaka
18, ni lazima ununue Omo 1kg moja ziwe pakti mbili au 500gm pakti ziwe nne au
3.5kg pakti moja,ambapo mshiriki utapewa kuponi ya itakayoingizwa kwenye droo
itakayochezesha kila jumamosi ya juma hilo.
Mwisho
Upendo aliwaomba wakazi wa jiji la Dar es Salaam kuchangamkia fursa ya pesa
hiyo kwani ushiriki na ushindi wake uko wazi.
Nikufanya
manunuzi ya Omo katika Supermakert ya Game,Choppies au Shoppers Mikocheni,
Msaki au Mbezi tayari unaweza kujishindia pesa taslimu Shilingi 500,000/=.
|
Post a Comment