CEO, Spotone Global Solution, Senegal and Member, Selection
Committee, Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP), Mariéme Jamme;
Director, TEEP, Parminder Vir; Founder, Tony Elumelu Foundation, Tony O.
Elumelu; CEO, Tony Elumelu Foundation, Reid Whitlock; CEO and Founder of Java
Foods, Zambia and Member, Selection Committee, TEEP, Monica Musonda; Founder
and Chair of Believe in Africa, Cameroon and Member, Selection Committee,
Angelle Kwemo during the official announcement of the selection of the first
1,000 African entrepreneurs for the Tony Elumelu Entrepreneurship Programme (TEEP) in Lagos
yesterday.
MFUKO wa Tony Elumelu (TEF) wenye makao makuu
yake hapa leo umetangaza orodha ya majina ya wajasiliamali 1,000 toka nchi 52
za Afrika walioshinda shindano maalumu la kuandika wazo la kukuza biashara au
kuanzisha biashara lililozinduliwa Januari 1 mwaka huu.
Jumla
ya washiriki 20,000 toka nchi 52 za kiafrika walishiriki shindano hilo ambao
waliwakilisha ubunifu na hazina iliyopo katika bara la Afrika. Kwa kuanza,
jumla ya washindi 1,000 wamechaguliwa kwa mwaka huu wa kwanza na washindi wote
wameonyesha uwezo wa kijasiliamali wa Kiafrika ambao utachochea ukuaji wa
uchumi na maendeleo kwa jumla.
Akiongea
manufaa ya mpango huo, Mwanzilishi wa Mfuko huo Bw Tony O. Elumelu, CON
alisema: “Uchaguzi wa wajasiliamali 1000 unatusogeza katika kufanikisha lengo
letu la kuchochea mageuzi ya uchumi na kijamii pamoja na kuongeza ajira barani
Afrika. Japokuwa sijakutana wala kuongea na mshindi yeyote, nina uhakika kwamba
kutokana na vigezo, washindi wote ni tumaini la Afrika ya baadaye. Nitandelea
kuwekeza uzoefu wangu, muda, ushawishi na rasilimali ili kupata mafanikio.
Nimeamua kuanza hii safari na hawa wajasiliamali nikiwa na matumanini na
mavuto.”
Washindi
hao wanawakilisha nchi 52 za Afrika na mipaka yake yote, ikiwemo sekta za
kilimo, elimu, mitindo na Tehama. Nchi tano za kwanza kuwa na washindi wengi ni
Nigeria, Kenya, Uganda, Afrika Kusini na Ghana. Kanda zote tano za Mashariki,
Kusini, Kaskazini na Magharibi ziliwakilishwa, zikiwemo kanda za waafrika
wanaoongea lugha za Kiingereza, Kifaransa, Kiarabu. Zaidi ya hapo,
wanatengeneza nafasi na ahadi kwa bara la Afrika.
Mfuko
wa Tony Elumelu uliichagua kampuni ya Accenture kama mhakiki huru wa kila kazi
iliyoshiriki kwa kuzingatia masharti na vigezo vilivyowekwa na kamati ya
uchaguzi ya mpango huo. Uhakiki huru na mkutano wa kamati ya shindano hilo
ulioshirikisha wajasiliamali na wataalamu wa maendeleo toka barani Afrika
hatimaye leo umetangaza washindi 1,000 wa shindano hilo.
Washindi
1000 waliotangazwa wataendelea na mafunzo mbalimbali kwa muda wa miezi tisa.
Mafunzo hayo ni pamoja na mafunzo kwa njia ya mtandao, mafunzo toka kwa
wajasiliamali waliofanikiwa na kambi za mafunzo.
Zaidi
ya washiriki 19,000 ambao hawakufanikiwa kwenye mchujo wa mwaka huu wataalikwa
kuingia katika mtandao wa wajasiliali wa Elumelu ambapo watajifunza mbinu
mbalimbali za kufanya biashara.
ParminderVir
OBE, Mkurugenzi wa Ujasiliamali kwenye Mfuko wa Tony Elumelu alisema: “Ushiriki
mkubwa na wenye kiwango cha hali ya juu tulioupokea ni ishara kuna vipaji
ambavyo vipo hapa Afrika. Mpango wa Ujasiamali wa Tony Elumelu (TEEF) utatoa
msaada kwa hawa wajasiliamali kujikuza
wenyewe pamoja na kuendeleza biashara zao. Kupitia mpango huu, manufaa ya muda
mrefu ya uwekezaji na kuzaliwa kwa kizazi kipya cha ubepari wa kiafrika
vinaweza kuenea bara zima la Afrika.”
|
Post a Comment