SAFARI LAGER YATANGAZA BAR 5 ZILIZOINGIA FAINALI SAFARI NYAMA CHOMA 2015 “DAR ONE”.
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza bar tano
zilizofanikiwa kuingia fainali kwenye kinyang’anyiro cha shindano la uchomaji
nyama Dar One lijulikanalo kama “Safari Lager Nyama Choma Competition 2015”.
Akizungumza na waandishi wa habari,
Meneja mauzo Tbl kwa ukanda wa Temeke, Patrick Swai alizitaja bar zilizoifanikiwa kuingia fainali
kuwa ni;
1.Kilwa road Bar.
2.Liquid Bar.
3.Chamanzi Bar.
4.Kwetu Pazuri Bar.
5.Minazini Bar.
Alisema Swai fainali za mashindano
ya Safari Nyama Choma mwaka huu wa 2015 zinatarajiwa kufanyika katika Uwanja TCC
Chang’ombe mkoani Dar es Salaam kwa kitongoji cha Dar One kama unavyojua kwa
mkoa huu wa Dar es Salaam tumeigawa katika sehemu mbili, Dar One na Dar two,
hivyo tunanza na Dar One jumapili hii ya
tarehe 29 Machi 2015 katika viwanja vya TCC Chang’ombe kuanzia saa mbili asubuhi na kuendelea tukisindikizwa
Bendi ya Msondo “Baba ya Muziki” pamoja
na DJ mkali kutoka hapahapa jijini Dar
es Salaam na burudani zingine nyingi pamoja na zawadi kemkem kutoka Safari
Lager..
Shindano hili hufanyika kila mwaka, na kwa mwaka huu linafanyika kwa mara ya nane mfululizo na mwaka huu mkoa wetu
tumekuwa wamwisho kuyafanya mashindano haya ambayo yalizinduliwa rasmi Mkoani
Mbeya wiki nnei zilizopita yakafuatiwa na Mwanza, Arusha na Kilimanjaro na sasa
ni Dar es Salaam.
Tangu lilipoanzishwa mwaka 2008,
shindano hili limekuwa na mvuto wa kipekee kwa wanywaji wa bia ya Safari Lager
kwani wamejitokeza kwa wingi kupigia kura baa zao kuhakikisha zinaibuka na
ushindi katika mkoa waliopo.
Kwa mwaka huu mchakato wa kuzipata bar
zilizoingia fainali ilikuwa ni wa kuipigia kura bar unayoipenda wewe mlaji wa
nyama choma kwa kutuma ujumbe mfupi wa maneno kutumia simu za mkononi kwenda
namba 0653-215151. Ujumbe ambao ulitozwa
gharama ya kawaida za kutuma ujumbe.
Alisema Swai “Lengo kuu la shindano
la Safari Lager Nyama Choma ni kuongeza
hamasa kwa watayarishaji na walaji wa nyama choma ili kwa pamoja waweze
kufahamu viwango bora vya uchomaji na utayarishaji wa nyama choma. Tunahakikisha
wachoma nyama katika baa za mikoa yote inayoshiriki wanapata elimu na ueledi wa
kutosha katika fani hii ili kumpa mlaji ubora anaostahili kila anapokula nyama
choma.
Tumezingatia maombi ya washiriki
mwaka jana hivyo basi mwaka huu semina inayoelekeza namna nzuri ya uchomaji
nyama itafanyika kwa bar zote zinazoshiriki na wala sio baa chache
zilizochaguliwa kama ilivyokuwa kwa miaka ya nyuma”. Swai aliendelea kufafanua
kwamba, washiriki watapimwa ujuzi wao katika kutayarisha nyama choma za aina
tatu; nyama ya ng’ombe, nyama ya mbuzi na nyama ya kuku.
“Safari Lager tutaendelea kujitahidi kuhakikisha
wateja wetu wanapata huduma bora ya nyama choma. Tunawaomba sana washiriki kutumia
vizuri elimu na uzoefu wanaopata ili kuongeza ubora wa utayarishaji wa nyama
choma kwa wateja wetu. Mashindano haya ya Safari
Lager Nyama Choma yatakosa maana sahihi endapo wachoma nyama watakuwa
wanashiriki kwa lengo la kujipatia manufaa binafsi na kusahau yale yote waliyojifunza
hadi mwaka mwingine”. Shindalo la mwaka huu linaongozwa na kibwagizo…. Safari Lager na Nyama Choma ndio Mpango
mzima!. Alisema Swai.
Mwisho Swai alitaja zawadi kwa kitongoji cha Dar One kuwa
ni;
1.Bingwa wa Mkoa ............... Kikombe na nafasi ya kushiriki fainali ya
Mkoa Leaders.
2.Mshindi wa pili
............... Nafasi ya kushiriki fainali ya Mkoa Leaders
3.Mshindi wa tatu ............... Nafasi ya kushiriki fainali ya Mkoa Leaders
4.Mshindi wa nne ................ 50,000/=
5.Mshindi wa tano ................ 50,000/=
Post a Comment