Mashabiki wa Bar ya Kill Home ya Moshi mjini wakishangilia kwa kucheza mara baada ya kutangazwa mabingwa katika mashindano ya Safari Lager Nyama Choma mkoani humo yaliyofanyika katika Uwanja wa Hogos zamani Pan African mwishoni mwa wiki.Bingwa alizawadiwa Kikombe na pesa taslimu Shilingi 1,000 000/=.
Na Mwandishi
Wetu.Moshi-Kilimanjaro.
KILL Home
Bar Moshi mkoani Kilimanjaro wameibuka mabingwa katika fainali za mashindano ya
Safari Lager Nyama Choma 2015 yaliyofanyiaka mswishoni mwa wiki katika Uwanja
wa Hugos zama ni Pan Africa na hivyo
kuzawadiwa fedha taslimu Shilingi milioni moja na Kikombe.
Nafasi ya
pili ilichukuliwa Rau Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi
800,000/=,nafasi ya tatu ni Makanyaga Bar ambayo ilizawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=,nafasi
ya nne ni Lamina Bar ambayo ilizawadiwa Shilingi 400,000/= na nafasi ya tano ni
White Star Bar ambayo ilizawadiwa Shingi 200,000/-
Akizungumza
na wakazi Moshi na vijitongoji jirani walifika katika mashindano hayo, Mkuu wa
Wilaya ya Moshi, Novatus Makunga, kwanza aliwashukuru kampuni ya Bia
Tanzania(TBL) kwa kuendea kudhamini mashindano ya Nyama Choma ambapo kwa mwaka
huu ni mara ya nane mfululizo kwani yamekuwa yenye mvuto wa pekee ambayo
yanawapa picha halisi wakazi wa Kilimanjaro kuwa wapi wanaweza kupata nyama
choma bora kutoka katika baa tano ambazo zimeingia fainali katika mkoa wetu.
Alisema Makunga
kwanza kabisa tunawapongeza kwa kutoa elimu kwa wapishi wa baa mbalimbali ambayo mliaanza nayo hapo awali tunaamini kwa
kupitia hilo wapishi wetu wameelimika si
kama mlivyowakuta na hilo tunawashukuru na tunawaomba muendelee nalo kwani
mnaongeza ajira kwa jamii kama si kupunguza umasikini.
Pili
aliwapongeza baa tano zilizoingia fainali kwani wao ndio baa bora katika baa
zote zinazochoma nyama mkoani humo na aliwaomba waendelee kuilinda hadhi na
sifa hiyo waliyopewa na mwisho
aliwapongeza mabingwa wapya Kill Home Bar kwa kutwaa ubingwa wa mashindano ya Safari
Nyama Choma kwa mwaka 2015 na kuwaomba ambao hawakufanikiwa kupata nafasi hiyo
wajiandae kwa mashndano yajayo ya Safari Nyama Choma 2016.
Nae Meneja
wa Bia ya Safari Lager, Edith Bebwa aliwapongeza mabingwa wa mwaka 2015,Kill
Home Bar na pia aliwashukuru wote
walioshiriki toka mchakato ulipoanza mpaka kufikia kumpata bingwa lakini pia aliwashukuru
wakazi wa Kilimanjaro waliojitokeza kwa wingi kuja kushuhudia nani anatwaa
ubingwa wa mashindano ya Safari Nyama Choma 2015.
Mwisho Edith
aliwaomba washiriki wote ambao waliopata zawadi wakatumie vyema zawadi
walizopata kwa kuboresha majiko yao kwa mashindano yajayo ya 2016 lakini pia
wakawe mabalozi wazuri wa bia ya Safari Lager kwenye biashara zao.
|
Post a Comment