Meneja wa
Bia ya Safari Lager, Oscar Shelikindo akizungumza na waandishi wa habari(hawapo
pichani) wakati wa kutangaza udhamini wa mashindano ya Safari All Afrika Pool Championships
yanayotarajiwa kuanza Octoba 16 mwaka huu katika Ukumbi wa Baudget Kunduchi
jijini Dar es Salaam. .Kulia ni Katibu Mkuu wa Chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos
Kafwinga na Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu.
 |
Katibu Mkuu
wa Chama cha Pool Taifa(TAPA), Amos Kafwinga akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) wakati wa Kampuni ya Bia Tanzania(TBL) kutangaza uzamani
wa mashindano ya Safari All Afrika Pool Championships yanayotarajiwa kuanza Octoba
16 mwaka huu katika Ukumbi wa Baudget Kunduchi jijini Dar es Salaam.Kushoto ni
Kocha wa timu ya Taifa, Denis Rungu na Meneja wa Bia ya Safari Lager, Oscar
Shelikindo.
KAMPUNI ya Bia Tanzania(TBL)
kupitia bia yake ya Safari Lager leo imetangaza kudhamini mashindano ya mchezo
wa Pool Afrika yajulikanayo kama “Safari
All Africa Pool Championship 2014.”
Akizungumza na waandishi wa habari, Meneja wa Bia ya
Safari Lager, Oscar Shelukindo alisema, “ Kwa mara nyingine tena bia ya Safari
Lager inashirikiana na Chama cha Pool nchini na Afrika kwa kudhamini Mashindano ya Pool Afrika 2014
yatakayotambulika kwa “Safari All Afrika Pool Championships. Tunafanya hivyo
ili kuhakikisha mchezo huu uanapanda na tunategemea timu yetu ya taifa itafanya
vizuri zaidi ya matokeo ya mwaka jana.”
Shelukindo alisema TBL kupitia bia ya Safari Lager
inawatakia kila la kheri timu ya Taifa kuanzia maandalizi mpaka mashindano
yenyewe tukiamini Ubingwa unabaki Tanzania lakini pia aliwakumbusha ujumbe
ambao tumekuwa tukiutumia kwa miaka kadhaa sasa wa “Play Pool Stay Cool” ambao hutukumbusha kuwa watulivu kila
tuchezapo na kumaliza.
Nae Mwenyekiti wa Chama
cha Pool Taifa(TAPA), Isack Togocho aliishukuru TBL kwa mara nyingine
tena kwa kudhamini mashindano hayo pamoja na timu ya Taifa ambayo kwa mara ya
kwanza Tanzania tunakuwa waandaaji.
Alisema Togocho hii ni dhahili kuwa mchezo wa Pool sasa
umekuwa Tanzania na kwa uandaaji huu tunaamini mwaka huu 2014 ushindi unabaki
Tanzania.
Katibu wa Chama cha Pool Taifa,Amos Kafwinga alizitaja
Nchi zinazoshiriki mashindano ya Safari
Pool Afrika kuwa ni Mabingwa watetezi wa mwaka jana, Zambia, Afrika Kusini,
Malawi, Lesotho, Kenya, Uganda, na wenyeji Tanzania.
Kafwinga alisema mashindano yatafanyika kwa siku tatu kuanzia
tarehe 16,17 na 18,2014 katika Ukumbi wa Budget Kunduchi jijini Dar es
Salaam.Timu kutoka katika nchi zote hizo tunatarajia zitaaanza kuwasili Octoba
15,2014.
Kuhusu timu ya Taifa ya Tanzania wanaendelea na mazoezi
kwa pande zote mbili ya Wanaume na Wanawake lakini rasmi wataingia kambini
Octoba 9,2014.
Meneja wa Bia ya Safari Lager alizitaja zawadi za
washindi kuwa ni
ZAWADI
|
TIMU/NCHI
|
SINGLE’S
WANAUME
|
SINGL’S
WANAWAKE
|
Mshindi wa Kwanza
|
5000$
|
2000$
|
1000$
|
Mshindi wa Pili
|
2000$
|
1000$
|
500$
|
|
Post a Comment