Meneja
wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edith Bebwa akizungumza na waandishi wa
habari(hawapo pichani) wakati wa uzinduzi wa mashindano ya mbio za Mitumbwi Kanda
ya Ziwa, zijulikanazo kama “Balimi Boat Race” iliyofanyiak Dar es Salaam
KAMPUNI ya Bia Tanzania (TBL) kupitia bia yake ya Balimi Extra leo imetangaza
rasmi kudhamini kwa mara nyingine tena mashindano ya mbio za mitumbwi kwa
wakazi wa kanda ya ziwa kwa mwaka huu wa
2014. Mashindano haya ya “kupiga
makasia” yanafanyika kwa mwaka wa kumi na tano sasa na yamekuwa na hamasa
na msisimko mkubwa kwa wakazi wa maeneo hayo.
Akizungumza na waandishi wa habari jijini Dar Es Salaam
leo, Meneja wa Bia ya Balimi Extra
Lager, Edith Bebwa alisema kwamba lengo hasa la Bia ya Balimi Extra
kudhamini mashindano haya ni kufurahi pamoja na wakazi wa kanda ya ziwa
hususani wale ambao ni wavuvi. Aliendelea kusema, “Mashindano haya yanaenzi na
kulinda tamaduni zetu zisipotee, yanajumuisha watu mbalimbali kukutana,
kufahamiana na kufurahi kwa pamoja na hii inasaidia sana kuimarisha amani na upendo
baina yetu. Amani ni nguzo muhimu sana kwa Taifa letu”. Alisisitiza pia umuhimu
wa michezo katika kujenga afya bora.
Edith alifafanua kwamba kwa mwaka huu mashindano ya mitumbwi
yatahusisha miji mitano ya kanda ya ziwa kama ratiba inavyoonyesha hapo chini
kwa hatua ya awali.
TAREHE
|
MAHALI/MKOA
|
UWANJA
|
18/10/2014
|
KIGOMA
|
UFUKWE WA MAGEREZA
|
01/11/2014
|
BUKOBA
|
UFUKWE WA SPICE BEACH
|
08/11/2014
|
MWANZA
|
UFUKWE WA MWALONI
|
15/11/2014
|
KISIWA CHA UKEREWE
|
UFUKWE WA HOTELI YA MONARCH
|
22/11/2014
|
MUSOMA
|
UFUKWE WA BWALO LA POLISI
|
Washindi watakaopatikana katika miji hii watashindanishwa
kwa pamoja ili kumpata mshindi wa kanda. Shindano la kumpata mshindi wa kanda
linategemewa kufanyika jijini Mwanza mwanzoni mwa mwezi December. Tarehe 6
Disemba 2014.
Edith Bebwa akizungumzia zawadi za mwaka huu alisema kwamba
katika ngazi ya mikoa na ngazi ya kanda Balimi Extra imetenga zaidi ya shilingi
milioni ishirini na nne kama zawadi za pesa taslimu kwa washindi. Mpangilio wa
zawadi ni kama inavyoonekana hapa chini;
ZAWADI
|
NGAZI YA MKOA
WANAUME
|
NGAZI YA MKOA
WANAWAKE
|
NGAZI YA KANDA
WANAUME
|
NGAZI YA KANDA
WANAWAKE
|
Mshindi wa Kwanza
|
900,000
|
700,000
|
2,700,000
|
2,300,000
|
Mshindi wa Pili
|
700,000
|
600,000
|
2,300,000
|
1,700,000
|
Mshindi wa Tatu
|
500,000
|
400,000
|
1,700,000
|
900,000
|
Mshindi wa Nne
|
400,000
|
300,000
|
900,000
|
700,000
|
Mshindi wa 5 - 10
|
6 @
250,000
|
6 @
200,000
|
6 @
400,000
|
6 @ 250,000
|
Edith alimaliza kwa kuwaomba wanachi wa kanda ya ziwa
wajitokeze kwa wingi katika miji iliyotajwa ili kufurahi kwa pamoja katika
matamasha haya. Alisisitiza wasisahau mila na tamaduni zao katika kipindi
ambacho watu wengi hupenda kuiga tamaduni za kimagharibi. Alimaliza kwa
kuwashukuru sana wanywaji wa bia ya Balimi Extra kwa kuchagua bia hii na kuomba
waendelee kuitumia kwani ni kupitia mchango wao ndipo pia Balimi Extra Lager
inaweza kuleta burudani kama hizi kwa ajili yao.
|
Post a Comment