Na Mwandishi Wetu.
KAMPUNI ya Samsung
inazindua rasmi duka kubwa na kituo chake cha huduma kwa wateja lililopo
barabara ya Sokoine mjini Arusha siku ya leo. Uzinduzi huo utawawezesha wateja
wake wote mkoani Arusha kupata huduma stahiki na bidhaa halisi za Samsung. Kituo
hiki ni cha kwanza kuzinduliwa mkoani Arusha na kampuni kubwa ya
kimataifa ya kielektroniki.
“Mtazamo wa maisha ya wateja hubadilika
kwa kasi kubwa na kuwafanya kuongeza mahitaji ya bidhaa na huduma bora. Kama
kampuni kubwa inayoongoza kuwa na vifaa bora vya kielektroniki ulimwenguni, Samsung
imefanya juhudi kubwa kuhakikisha inatimiza mahitaji ya wateja wake wote Afrika.
Mkoa wa Arusha hutegemea sana biashara kwani una wakaazi toka jamii
mchanganyiko. Hivyo katika Afrika Mashariki, Arusha ni kitovu cha wageni toka
nchi mbalimbali ulimwenguni. Kampuni ya Samsung ina imani kubwa kwamba kituo
cha huduma kwa wateja kitatoa ushirikiano mzuri na kuboresha uhusiano kwa wateja
wake mkoani Arusha. Kwasababu Arusha ni kituo kikuu cha safari nchini
Tanzania”, haya yamesemwa na
Mkurugenzi mkuu wa kampuni hii nchini Tanzania, Bw. Seo
Kituo
hiki kitatoa huduma za ziada kwa wateja wa Samsung mbali na kuuza simu za
mkononi na bidhaa za kielektroniki. Hii ni pamoja na kuwapa wateja wake
watakaojisajili na huduma ya e-warranty
(dhamana) usaidizi wa kiufundi bila malipo kwa kipindi cha miaka miwili.
Mpango
huu utawanufaisha wateja wa Samsung watakaosajili bidhaa zao kupitia Simu. Huu
ni mchakato utakaofanyika kwa kutuma namba ya IMEI kwenda 15685. Baada ya
kufanya hivyo wateja watanufaika na msaada wa kifundi kwa kipindi cha miaka
miwili sambamba na kujipatia nafasi ya kushinda bidhaa mbalimbali za Samsung.
Katika
kusherehekea uzinduzi wa kituo cha huduma kwa wateja ambacho kinawasogezea
wateja wake huduma karibu, kampuni hii kubwa duniani inawaletea habari njema
wakaazi wa Arusha kwa kutoa punguzo kubwa la bei za bidhaa zake. Kwenye kipindi
hiki cha ufunguzi bidhaa zitakazokuwa na punguzo la bei ni pamoja na; Luninga, feni,
majokofu na vifaa vya nyumbani. Bila kuwasahau wateja wake wa simu, vifurushi
vya intaneti na zawadi za T-shirts zitatolewa kwaajili ya wanunuzi wa simu aina
ya Galaxy Trend lite.
Kwa sasa nchini Tanzania
kampuni ya Samsung ina maduka na vituo vya huduma kwa wateja katika mikoa ya
Mwanza na Dar es Salaam na ina mipango kabambe kuongeza huduma zake mikoa
mingine.
Duka hili na kituo chake
cha huduma kwa wateja vitatoa huduma siku za wiki yaani Jumatatu-Ijumaa kuanzia
saa 9.30 asubuhi hadi 5.00jioni kwa Jumamosi ni kuanzia saa 9.30asubuhi hadi
1.00 mchana, litafungwa siku za Jumapili na Siku kuu.
|
Post a Comment