Baadhi
ya wacheza ngoma wa kikundi cha Bujora wakishangilia na kikombe pamoja na pesa
taslimu shilingi 1,100,000/= mara baada ya kuibuka mabingwa wa Kanda ya Ziwa wa
fainali za mashindano ya Ngoma za Asili yalifanyika katika Uwanja wa Mabatini
jijini Mwanza.
Bujora mabingwa Balimi Ngoma Kanda ya
Ziwa 2014.
Na Mwandishi
Wetu.
KIKUNDI cha
Ngoma za asili cha Bujora cha jijini Mwanza kimefanikiwa kuchukua ubingwa wa
fainali za mashindano ya Ngoma za asili kanda ya ziwa mwishoni mwa wiki kwa pointi 87.5 zilizofanyika katika Uwanja wa
Mabatini kwa kushirikisha mabingwa
wawili kutoa katika mikoa mitano ambayo ni Tabora, Shinyanga, Kagera,Mara na
Mwanza.
Kwa ubingwa
huo kikundi cha Bujora kilizawadiwa pesa taslimu shilingi 1,100,000/= , kikombe
pamoja na medali za dhahabui cha Mwanalyaku ambao walipata pointi .
Nafasi ya Pili katika fainali hizo
ilichukuliwa na kikund Mwanalyaku cha jijini Mwanza pia kwa pointi 79.5 na
hivyo kuzawadiwa pesa taslimu shilingi
850,000/=
Nafasi ya
tatu ilichukuliwa na kikundi cha Bugoloile cha Kagera kwa pointi 79.3 na hivyo
kuzawadiwa pesa taslimu Shilingi 600,000/=.Nafasi ya nne ilikwenda kwa kikundi
cha Mabulo ya Jeshi cha Sinyanga kwa pointi 76.7 na hivyo kuzawadiwa pesa
taslimu Shilingi 500,000/=.
Nafasi ya
tano mpaka ya kumi ni kikundi cha Rugu kagera pointi 75.2,Musoma One cha Mara
73.8,Wanunguli Shinyanga pointi 73.1,Magereza Tabora 70.1,Kiwajaki Mara 69.6 na
cha mwisho ni kikundi cha Bugobogobo cha Tabora pointi 59.3.
Mgeni rasmi
katika fainali hizo alikuwa Kaimu Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Mwanza,
Christopher Fuime ambaye aliishukuru Kampuni ya Bia Tanzania kwa kuzamini
mashindano ya ngoma ambayo hufanyika kila mwaka wakati wa mavuno ambapo
aliwaomba waendelee kudhamini kwani yanatukumbusha asili yetu tulikotoka na pia
zawadi wanazopata zinaongeza kipatao kwa washiriki.
Nae Meneja
wa Bia ya Balimi Extra Lager, Edithi Bebwa aliwashukuru washiriki wote kwa kuwa
mabingwa wa mkoa yao huko wanakotoka na pia aliwashukuru kwa kushiriki fainali
za Kanda na kuwaahidi kuboresha zaidi mashindano mwaka ujao hasa upande wa
zawadi.
Edithi
alisema sababu msinigi ya kuwepo kwa Mashindano ya Balimi Ngoma za
Asili ni kuenzi na kulinda utamaduni wa Kitanzania.
Kampuni ya Bia nchini ni sehemu yao ya kurudisha fadhila
kwa watumiaji wa Kinywaji cha Balimi Extra Lager pamoja na vinywaji vyote vya
Kampuni ya Bia Tanzania(TBL).
|
Post a Comment