ad

ad

MWEZI AGOSTI: MENEJA BORA BRENDAN RODGERS, MCHEZAJI BORA DANIEL STURRIDGE!!

Barclays Wadhamini wa ligi kuu England leo wametangaza waliozoa Tuzo ya Mwezi Agosti ya Ligi hiyo ya Meneja na Mchezaji Bora na wote wanatoka Liverpool.

Meneja Bora ni Brendan Rodgers na Mchezaji Bora ni Straika Daniel Sturridge.

Kwa sasa Liverpool ndio Vinara wa Ligi Kuu England baada ya kushinda Mechi zao zote 3 za mwanzo kwa Bao 1-0 katika kila Mechi na Mfungaji wa Bao zote hizo 3 ni Daniel Sturridge.
Liverpool walianza Ligi kwa kuzifunga Stoke City na Aston Villa Mwezi Agosti na Man United Mwezi Septemba.
Hii ni mara ya Pili kwa Brendan Rodgers kutwaa Tuzo hii na ni mara ya kwanza kwa Sturridge.
Meneja ambaye anaongoza kwa kutwaa mara nyingi Tuzo hii ni Sir Alex Ferguson aliekuwa Manchester United alietwaa mara 27 akifuatiwa na Arsene Wenger wa Arsenal mara 12 na David Moyes, ambae sasa yupo Man United, alipokuwa Everton mara 10.
Kwa upande wa Wachezaji, wanaoongoza kwa kutwaa mara nyingi ni Wayne Rooney, Robin van Persie na Steven Gerrard ambao wote wametwaa mara 5 kila mmoja lakini Mchezaji pekee aliewahi kuitwaa Mara nyingi katika Msimu mmoja ni Ashley Young alietwaa Mara 3 kwenye Mwaka 2009 akiwa na Aston Villa.
Manchester United ndio inaongoza kwa kutoa Washindi wengi wa Tuzo hii.Ukabaji wa Liverpool wiki iliyopita walipoifunga United bao 1-0

No comments