Mh. Lowassa asimikwa kuwa Chifu wa Unyanyembe Mkoani Tabora leo,pia aweka jiwe la msingi Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi
.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa akivishwa vazi maalum la Kichifu
pamoja na kukabidhiwa Mkuki na Chifu Mkuu wa Kabila la Unyenyembe,Chifu
Msagata Fundikira ikiwa ni ishara ya kumsimika kuwa Chifu wa Kabila
hilo,wakati wa Sherehe za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike
Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika
jana kwenye Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa (kulia) akisikiliza kwa makini
Wasifu wa Marehemu,Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki Miaka 124
iliyopita.Wasifu huo Ulisomwa na Bw. Richard Mchembe.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la
Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakishirikiana kuweka jiwe la msingi
katika eneo litakalojengwa Mnara wa kumuenzi Mtemi Isike Mwanakiyungi
aliefariki Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye
Kijiji cha Itetemya,Mkoani Tabora.
Waziri Mkuu Mstaafu na Mbunge wa
Jimbo la Monduli,Mh. Edward Lowassa pamoja na Chifu Mkuu wa Kabila la
Unyenyembe,Chifu Msagata Fundikira wakiwa kwenye picha ya pamoja na
Machifu kutoka mikoa mbali mbali hapa nchini walioshiriki kwenye Sherehe
za Maadhimisho ya Kumbukumbu ya Mtemi Isike Mwanakiyungi aliefariki
Miaka 124 iliyopita.Sherehe hizo zimefanyika jana kwenye Kijiji cha
Itetemya,Mkoani Tabora. BOFYA HAPA KUONA PICHA ZAIDI
Post a Comment