MABINGWA WA MKOA WA MOROGORO WA SAFARI POOL,ANATORY POOL CLUB,WATAMBA KUTWAA UBINGWA SAFARI POOL NATIONAL CHAMPIONSHIP 2013.
Nahodha wa klabu ya Anatori, Athumani Selemani(kulia) na Harid Mohamed wakishindana kulagi wakati wa mazoezi wakijiandaa na fainali za mashindano ya Pool Taifa yanayotarajiwa kufanyika Mkoani Morogoro Septemba 19-22,2013 katika ukumbi wa Tanzanite.
Nahodha wa klabu ya Pool ya Anatory,Athumani Selemani akilagi |
Harid Mohamed akicheza
ANATORY WATAMBA KUTWAA UBINGWA WA
SAFARI POOL TAIFA 2013.
MKURUGENZI
wa Klabu ya mchezo wa Pool ya Anatory, Anatory Makasi ametamba kutwaa Ubingwa
wa fainali za mashindano ya Pool Taifa kwa mwaka huu wa 2013.
Anatory
ameyasema hayo leo wakati klabu yake ikifanya mazoezi kambini Old View Hotel iliyopo Morogoro kujua maandalizi yake kama mwenyeji wa fainali
za mashindano ya Safai Pool Taifa 2013, ambayo kwa mwaka huu yanatarajiwa
kufanyika mkoani Morogoro.
Anatory
amesema anakilasababu za kutwaa ubingwa huo kwani amejiaandaa vizuri,alikuwa na
kambi katika mikoa tofauti ikiwemo Dodoma na Taanga na sasa vijana wako kambini
wakiendelea na mazoezi makali kuikabili mikoa 16 ikiwakilishwa na vilabu 16 vinavyotarajiwa
kuwasili kuanzia Septemba 15 na 16 wiki ijayo.
Alisema
Anatory vijana wako vizuri hawana shida kabisa wanachosubiri ni kukamilisha
adhima yao ya kutwaa Kikombe na na fedha taslimu shilingi 5,000 000/= kama mabingwa wa “Safari Pool National
Championship 3013”.
Mkurugenzi
Anatory alimaliza kwa kuwatoa hofu wageni watarajiwa kuwa Morogoro pako
swari,amani tele,usalama upo wa kutosha,hali ya hewa nzuri kabisa hakuna joto
hivyo wachezaji wote pamoja, viongozi na mashabiki wanakaribishwa Morogoro.
Nae Nahodha
wa Klabu ya Anatory,Athuman Selemani alikitaja kikosi chake anachokiongoza kuwa
ni Harid Mohamed,Six Timbulo,Alfan Ngassa,Juma Kassim,Juma Ally,Charles Philipo
na Mussa Mkwanga.Ambapo viongozi ni Mwenyekiti Jackson Philipo,Katibu Mohamed
Makanyaga na Mkurugenzi Anatory Makasi.
Fainali za
Safari National Pool 2013 zinashirikisha mikoa 17 ambayo ni Morogoro
wenyeji,Lindi,Kagera ,Tabora,Mwanza
Shinyanga,Morogoro,Arusha,Kilimanjaro,Tanga,Manyara,Pwani,Temeke,Ilala,Kinondoni,Dodoma,Iringa
na Mbeya.
Harid Mohamed alishinda frame hiyo.
Post a Comment