HAFSA KAZINJA AIBUKA KIVINGINE AKIMUENZI NGURUMO
Malkia wa Zouk nchini Hafsa Kazinja(katikati) akiwa na Omari Mkali
(kushoto) na Abdul Salvador baada ya kukamilisha kurekodi wimbo wa 'NIMUOKEOE
NANI' katika Studio za OM Productions jijini Dar es salaam .
Omari Mkali akimuwekea mic vizuri
Na Mwandishi Wetu.
MALKIA wa
Zouk Tanzania, Hafsa Kazinja, anaibuka upya katika fani akiwa
na ingizo lake la kwanza kati ya kumi aliyoandaa kwa kuimba wimbo maarufu
wa NUTA Jazz Band uitwao “NIMUOKOE NANI” anauouleta hewani katika mahadhi
ya Zouk.
Hafsa Kazinja anasema ameamua kurudi ulingoni kwa kutoa
wimbo huo ili kumuenzi Mzee Muhidin Maalim Gurumo ambaye amestaafu rasmi fani
ya muziki baada ya kufanya kazi hiyo akiwa na bendi mbalimbali tokea mwaka wa
1960.
“Nimeamua kuimba wimbo huu wa “NIMUOKOE NANI” ili
kumuenzi gwiji huyu wa muziki kwani wakati yeye anastaafu na mimi ndiyo
naibuka upya baada ya kukaa kimya kwa muda”, anasema Hafsa ambaye alitoka kwa
wimbo wake wa “PRESHA” aliomshirikisha Banana Zorro.
Hafsa ameandaa wimbo huo wa “NIMUOKOE NANI” katika studio za
OM Productions ya jijini Dar es salaam chini ya wanamuziki nguli, Abdul
Salvador na Omari Mkali.
“Nafurahi kwamba wimbo wa NIMUOKOE NANI nimeuimba baada ya
kupata Baraka zote toka kwa mtunzi na mwimbaji wake Mzee Gurumo mwenyewe.
“Haikuwa rahisi kama inavyoweza kudhaniwa kwani baada ya
kwenda kumuona nyumbani kwake alinifanyisha mtihani wa kuuimba wote kabla ya
kuridhika maana alisema asingefurahi kuona wimbo wake unaimbwa hovyo hovyo na
kuharibiwa radha yake”, anasema Hafsa, ambaye hivi sana anamalizia ngoma zake
zingine tisa alizotunga mwenyewe, kabla ya kuvamia anga kwa mara ingine.
Hafsa anasema katika ukimya wake amekuwa akifanya utafiti na
kujifunza kwa undani zaidi fani ya muziki, akipata mawaidha maridhawa toka kwa
wanamuziki nguli ndani nan je ya nchi wakiwemo Muhidin Maalim Gurumo, Omar
Mkali, Abdul Salvador na Lokassa ya Mbongo wa Congo aliyekutana na kufanya naye
kazi alipokuwa ziarani Marekani hivi karibuni.
Msanii huyu wa kizazi kipya anasema ataitambulisha rasmi
ngoma ya “NIMUOKOE NANI” katika tamasha la kumuenzi Mzee Gurumo lililopangwa
kufanyika OKtoba 1, 2013 katika ukumbi wa Diamond Jubilee jijini Dar es salaam.
“Natumaini wapenzi wa muziki watafurika kwa wingi kwenye
tamasha hilo name naahidi kuitendea haki ngoma ya “NIMUOKOE NANI” hivyo
wasikose kuja kujionea wenyewe jinsi sie wa kizazi kipya tunavyoweza kufanya
kazi na wakubwa wetu wa kazi, anaongezea Hafsa ambaye pia anaandaa video yake
pamoja na ya ngoma zake zingine mpya.
Mkongwe Abdul Salvador, ambaye alikuwa mmoja wa waanzilishi
wa bendi ya TANCUT ALMASI YA Iringa iliyotamba na mtindo wake wa “FIMBO
LUGODA”, anamtaja Hafsa kazinja mmoja wa wanamuziki wa kike waliojaaliwa sauti
nzuri na kipaji cha hali ya juu hapa nchini.
“Kwa kuweza kuimba wimbo wa Mzee Gurumo na kupatia
kisawasawa inadhihirisha kwamba Hafsa ni mwanamuziki aliyekomaa maana si mchezo
kuimba nyimbo ya wakongwe kwa ufasaha kama alivyofanya Hafsa.
“Na hii inadhihirisha kwamba uwezekano wa kizazi kipya na
cha zamani kufanya kazi pamoja ni mkubwa sana na sioni kwa nini isiwe hivyo”,
anasema Salvador.
Post a Comment