UBA YAZINDUA HUDUMA YA U- MOBILE TANZANIA.
Mwenyekiti
wa Bodi wa Benki ya Unite Bank of Afrika(UBA), Generali Mstaafu, Robert
Mboma(kushoto) na Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo, Demola Ogunfeyimi(wa pili
kushoto) wakipongezana mara baada ya kuzindua huduma mpya ya U-mobile kwa benki
hiyo iliyofanyika Dar es Salaam jana.Kushoto ni Meneja wa Benki hiyo Nchini Tanzania, Dinko
Svetic na Mkuu wa Oparesheni wa Benki hiyo, Chis Byaruhanga wakipiga makofi na
wa kwanza kulia ni Mkuu wa Mauzo na masoko wa benki hiyo, Julius Konyani.
Mwenyekiti wa Bodi wa Benki ya Unite Bank of Afrika(UBA), Generali Mstaafu, Robert Mboma akikata utepe kuashira uzinduzi huo.
Wasanii wakicheza wakati wa uzinduzi huo.
Baadhi ya Wafanyakazi wa Benki hiyo na wageni waalikwa wakifuatilia uzinduzi huo.
Mkurugenzi mtendaji wa Benki hiyo, Demola Ogunfeyimi akizungumza wakati wa uzinduzi huo.
BENKI ya UBA Tanzania (United Bank for
Africa) leo hii imezindua huduma mpya ya U- Mobile katika ofisi zao kuu jijini
Dar es Salaam. Wateja wa Benki hiyo wanaweza kupata huduma hiyo mara moja kwa
kujiandikisha na kupata huduma kwenye simu ya mkononi na vifaa vya umeme.
UBA ni Benki ya kwanza kuwa na huduma
yake ya simu kupatikana katika katika majukwa 2 tofauti: kupitia App ya simu ya
mkononi kwa wale ambao wana smart phone na pia kupitia mfumo wa USSD code,
ambayo inapatikana kwa watu wote kwa kujisajili kupitia *150*77#.
Kwa kutoa huduma ya U- Mobile, Benki
hiyo inawapa wateja wake njia rahisi ya kupata na kusimamia fedha zao. Pia
kupitia U- Mobile wateja wa UBA watapata zaidi ya huduma 14 zikiwemo; uhamisho
wa fedha, usimamizi wa fedha, kununua salio, kulipia huduma za: LUKU, DSTV,
kununua tiketi nk.
Akizungumza na waandishi wa Habari
katika uzinduzi huo, Mkurugenzi Mtendaji wa UBA Tanzania, Demola Ogunfeymi,
alisema, “Tunafurahi sana kuweza kuwapa watanzania huduma hii kwa mifumo ambayo
inawafa, nia yetu ni kuwapa wateja wetu suluhisho bunifu na rahisi la
kuwawezesha kusimamia fedha zao”.
Naye Mwenyekiti wa UBA Tanzania, Jen.
Robert Mboma, alisema, “Nia ya benki hii kutoa na kuhakikisha bidhaa na huduma
kwa wateja ni ya kipekee na ni ya hali ya juu”.
Mkuu wa Bidhaa wa UBA Tanzania, Julius
Konyani alisema kwamba benki hiyo imeweka mikakati ili kuhakikisha akaunti za
wateja zinabaki salama. Aliendelea kusema, “Tuna timu ambayo inawajibika na
usimamizi wa huduma ya U- Mobile na kutoa msaada masaa 24 kwa siku, siku 7 kwa
wiki”.
Huduma hii inapatikana kwa wateja wetu
ambao wana akaunti za XXX na Akiba au kadi ya UBA Prepaid na ni lazima kwanza
wakamilishe fomu za kujiandikisha zinazopatikana katika matawi ya yote ya benki
ya UBA. Mchakato huu ni wa haraka na rahisi kwani maelezo yote yanapewa kwa
mteja ili aanze kutumia huduma hiyo haraka.
Mkuu wa Mauzo na masoko wa benki hiyo, Julius Konyani akizungumza.
Post a Comment